Magufuli aliua fastjet ila Mungu anamuona nilikaa zaidi ya miaka 3 bila kupanda basi za mikoani, ila sasa hao wa Air Tanzania ni bogus safari zao ni kubahatisha tu.Nimejikuta nazikumbuka sana monents za Fast Jet miaka ya 2010's
Ni kipindi nachoweza kusema nilitoa ushamba wa ndege, ndege ilikuwa kama basi la mkoani.
Ilikuwa ni mkombozi mkubwa sana kwa watu wenye uchumi wa kawaida.
Ndege zilikuwa zinajaa inabidi ukate ticket mapema,
Nilichokuwa nawapendea nje ya bei rafiki ni kujali ratiba, ukifika uwanjani una uhakika wakuondoka muda uliopangwa.
Tangu Fastjet waondoke nimepanda ndege mara 2 tu, moja ni emergency nyingine ni kikazi [emoji23][emoji23]