Tangazo la Makonda, nafasi ya Mkuu wa Mkoa ni ipi?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,848
730,361
Habari ya walimu wa Dar kusafiri bure kupitia tangazo la mkuu wa wilaya ya Kinondoni ni muingiliano wa madaraka.

Inawezekana kabisa Makonda kajisahau na kudhani yeye ni mkuu wa mkoa.

Kiutaratibu alipaswa kuwasemea watu wa eneo lake tu la kiutawala ama la angekutana na wakuu wa wilaya wenzake wa Ilala na Temeke na kutoa tamko la pamoja au wangeonana na bosi wao mkuu wa mkoa yeye ndio aseme kwa niaba ya wote.

Ila kwakuwa Makonda sio mtu wa tafakuri na mpenda sifa tusubiri mkanganyiko kwenye hili hasa itakapotokea kwa walimu wa wilaya nyingine kutaka kupanda bure mabasi ya eneo lao.

Kuna hili la vitambulisho, je vitatolewa na mamlaka gani? Kwakuwa Makonda hana mandate ya kusaini vitambulisho vya mkoa wa dsm bali Kinondoni tuu kwakuwa yeye si RAS.

Hili ni zoezi la mlipuko lenye kukurupuka kwingi, lisilo na misingi ya mgawanyo wa madaraka na utawala wa sheria litakaloleta mgongano mkubwa wa kimaslahi.
 
Navyojua makindakta walivyo wakuda watawadhalilisha sana walimu..kimsingi hili jambo halina maana ni kujifanya unabuni vitu ambayo haviwezi kuwa endelevu..kinachotakiwa ni kuweka miji vizuri mwalimu akae jirani na shule yake na miundombinu iwepo lakini hii ya bure bure ni kudhalilisha watu tu...
 
Habari ya walimu wa Dar kusafiri bure kupitia tangazo la mkuu wa wilaya ya kinondoni ni muingiliano wa madaraka
Inawezekana kabisa Makonda kajisahau na kudhani yeye ni mkuu wa mkoa. Kiu taratibu alipaswa kuwasemea watu wa eneo lake tu la kiu tawala ama la angekutana na wakuu wa wilaya wenzake wa Ilala na Temeke na kutoa tamko la pamoja au wangeonana na bosi wao mkuu wa mkoa yeye ndio aseme kwa niaba ya wote
Ila kwakuwa Makonda sio mtu wa tafakuri na mpenda sifa tusubiri mkanganyiko kwenye hili hasa itakapotokea kwa walimu wa wilaya nyingine kutaka kupanda bure mabasi ya eneo lao...!
Kuna hili la vitambulisho je vitatolewa na mamlaka gani? Kwakuwa Makonda hana mandate ya kusaini vitambulisho vya mkoa wa dsm bali kinondoni tuu kwakuwa yeye si RAS
Hili ni zoezi la mlipuko lenye kukurupuka kwingi, lisilo na misingi ya mgawanyo wa madaraka na utawala wa sheria litakaloleta mgongano mkubwa wa kimaslahi
Mwendelezo wa siasa za kiramliramli,kichawi chawi,fisi fisi...jukumu la Makonda ni wilaya ya Kinondoni na amesimamia hilo kwa kinondoni sasa kama litaonekana jema kwa Dar nzima safi tu...tulilalamika sana kwamba viongozi hawawajibiki sasa tunakuja na hoja potofu kufifisha maendeleo.
 
mshana jr nadhani ingekuwa busara kama ungetofautisha majukumu ya kiserikali na mambo binafsi. Suala la kupanda walimu bure halihusiani na mambo ya kiserikali wala majukumu ya kiutawala ya mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa. Alichofanya Mh. Makonda ni kutumia mahusiano yake na wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwaomba wawasafirishe walimu bila kuwatoza nauli. Lile ni ombi binafsi la Makonda na wala si sheria wala amri iliyotolewa na serikali.
 
Kwahiyo hata vitambulisho atasaini yeye kwa walimu wote wa Dar?
 
Mkuu vipi leo umeamka na viroba? Makonda katangaza walimu kusafiri bure wilayani kwake kinondoni hajasema mkoa wa Dar es salaam!!!!!!!!!!
Hahhahahaaaa hebu njoo kule kwenye post nyingine uone uongo wako...niliposema mkanganyiko ndo kama huu sasa kwahiyo sio walimu wa dar ni wa kinondoni pekee? Msaada hapa tafadhali
 
Kwahiyo hata vitambulisho atasaini yeye kwa walimu wote wa Dar
Mshana unaabisha Makonda kaongelea kinondoni sio Dar ni kwa ajili ya walimu wanaofundisha kinondoni.Hivyo vitambulisho huko wanakofundisha ndiko watawasaidia.Umeshupalia DAR,DAR hivi hufuatilii hata vyombo vya habari? uSISEME TENA WALA KUANDIKA DAR andika kinondoni.
 
Hahhahahaaaa hebu njoo kule kwenye post nyingine uone uongo wako...niliposema mkanganyiko ndo kama huu sasa kwahiyo sio walimu wa dar ni wa kinondoni pekee? Msaada hapa tafadhali

Ni walimu wa kinondoni tu sio dar es salaam nzima
 
Mshana unaabisha Makonda kaongelea kinondoni sio Dar ni kwa ajili ya walimu wanapfundisha kinondoni.Hivyo vitambulisho huko wanakofundisha ndiko watawasaidia.Umeshupalia DAR,DAR hivi hufuatilii hata vyombo vya habari? uSISEME TENA WALA KUANDIKA DAR andika kinondoni.
Ngoja nitakutag mahali uje ujionee na kama kamaanisha kinondoni tu wakati huo huo kakubaliana wa wamiliki wa vyombo vya usafiri dar nzima hii nayo ikoje?
 
Mwalimu mwenyewe atakayesafiri bure anatakiwa kuwa mvumilivu wa kuvumilia matusi na awe hana aibu vinginevyo kama una aibu lazima ulipe nauli.
Aibu gani? Mbona askari fresh tu pamoja na maneno ya kejeli ya hapa na pale na kama elimu ya yule jamaa'ko.
Taratibu mpaka watu wanazoea,tatizo lingine nyie Nyumbu roho inawauma sana vitu vizuri vinavyokuwa initiated na majembe ya chama tawala lakini ingekuwa mmeasisi nyie mngetetea mpaka basi.
Nyambaffff sana nyie
 
Ngoja nitakutag mahali uje ujionee na kama kamaanisha kinondoni tu wakati huo huo kakubaliana wa wamiliki wa vyombo vya usafiri dar nzima hii nayo ikoje?

Hivi kisichoeleweka hapo ni nini? CHAMA cha wamiliki wa daladala DAR huwezi kuongea nao wakusaidia kusafirisha walimu bure wilaya mojawapo au mtaaa fulani wa dar es salaam? Unachofanya ni kuwaomba waongee na wanachama wao wa eneo fulani wasafirishe bure.Tatizo liko wapi?
 
Nikiwa kwenye daladala asubuhi hii pembeni yangu alikaa binti mmoja .Mara konda akaanza kudai nauli,nikamuona binti kafungua pochi yake na kutoa kitambulisho kisha kumkabidhi konda,nikamsikia konda akisema "KUMBE HATA WEWE NI MWALIMU!"binti akakaa kimya akarudishiwa kitambulisho chake na hakulipa nauli.
 
Hivi kisichoeleweka hapo ni nini? CHAMA cha wamiliki wa daladala DAR huwezi kuongea nao wakusaidia kusafirisha walimu bure wilaya mojawapo au mtaaa fulani wa dar es salaam? Unachofanya ni kuwaomba waongee na wanachama wao wa eneo fulani wasafirishe bure.Tatizo liko wapi?
Hebu kasome The Phylosopher alichoandika
 
Back
Top Bottom