Tangazo la kuuza nyumba za mfuko wa pspf

engmtolera

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
5,149
Reaction score
1,441
1.jpg

34.jpg

2.jpg

6a.jpg

chanzo cha picha ni http://mitaa-yetu.blogspot.com/2013/02/mikopo-nyumba-pspf.html

Mfuko wa Pensheni wa PSPF unapenda kuutaarifu Umma kuwa umezindua Mpango Mpya wa uuzaji nyumba zake zilizojengwa kwa ajili ya makazi katika mikoa ya Dar es Salaam- Ilala (Buyuni), Morogoro (Lukobe), Tabora (Usule), Mtwara (Mang'amba), Shinyanga (Ibadakuli) na Iringa (Mawelewele).

Bei za nyumba ni kati ya sh. 52,000,000.00 hadi sh. 71,000,000.00 (bila VAT). Bei hizi ni kulingana na ukubwa wa nyumba na mkoa nyumba ilipo. Ukubwa wa nyumba ni kuanzia vyumba viwili hadi vinne.

Chini ya utaratibu huu mpya unaoanza kutumika kuanzia Februari 2014; Muombaji atapaswa kuainisha kwenye fomu ya maombi aina ya nyumba anayohitaji na Mkoa ilipo. Malipo yanaweza kufanyika kwa njia zifuatazo:

1) UNUNUZI KAMA MPANGAJI (HIRE PURCHASE):
Mnunuzi atalipia kwa mpango wa mwezi mmoja mmoja au miezi mitatu kwa mkupuo (installments) kulingana na thamani ya nyumba. Katika mpango huu, mnunuzi anaweza kulipia kutokana na vyanzo vingine vya mapato yake mbali na mshahara wake. Mwanachama wa PSPF aliyechangia chini ya miaka mitano (5) atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 5,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba na asiye mwanachama wa PSPF atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 10,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba kukidhi vigezo vya kununua nyumba (kama mpangaji).

Mpango huu wa Ununuzi kama Mpangaji (Hire Purchase) utamwezesha mnunuzi kulipa kati ya sh. 450, 000.00 (laki nne na hamsini tu) na sh. 813,000.00 (laki nane na kumi na tatu tu) kwa mwezi kama malipo ya nyumba zinazouzwa na Mfuko kulingana na ukubwa na eneo nyumba ilipo.

2) MALIPO YA MARA MOJA (OUTRIGHT PURCHASE)
Mnunuzi atalipia gharama ya kununua nyumba kupitia akaunti ya Mfuko na kisha kusaini makubaliano kabla ya kuhamishiwa umiliki (transfer).

3) MKOPO WA NYUMBA KUPITIA BENKI (MORTGAGE BASIS):
Mnunuzi anaweza kuchukua mkopo katika mojawapo ya Benki ambazo Mfuko wa PSPF ina mikataba nazo na kutumia mkopo huo kununulia nyumba. Mabenki hayo ni; CRDB, Azania, Exim na NMB.

MUHIMU! Iwapo utanunua nyumba kupitia mkopo wa benki (Mortgage) utapaswa kuwa umesajiliwa kwenye Mfuko na kuchangia kwa muda wa miaka mitano au zaidi. Muda wa kurejesha mkopo ni mpaka miaka ishirini na mitano (25) kulingana na matakwa ya Benki husika.

Mwombaji anayehitaji kuona au kukagua nyumba awasiliane nasi kupitia simu: +255 22 2120912/52 au +25522 2127375-6 au E-mail: pspf@pspf-tz.org.
Kwa maelezo zaidi fika Makao Makuu ya PSPF yaliyopo jengo la Golden Jubilee Towers, Barabara ya Ohio au ofisi zetu zilizopo katika kila mkoa.
Imetolewa na

Mkurugenzi Mkuu,

Mfuko wa Pensheni wa PSPF
 
engmtolera, wewe ndo afisa habari wa PSPF? Au umejitolea tu kuleta hili tangazo hapa
 
Last edited by a moderator:
engmtolera, wewe ndo afisa habari wa PSPF? Au umejitolea tu kuleta hili tangazo hapa

we una taka kuona tangazo toka kwa mwenye mbwa ama mbwa mwenyewe hahahahaha
mimi nimelikuta huko mitaani na kulileta hapa,maana wenye mapasi pia wamo humu JF,kwa hiyo mnaweza jipatia nyumba hizo bila shaka
 
DAHHizo nyumba ni zile za CHANIKA KIGEZI! HAPANA JAMANI MNATUNYONYA ZZILE NYUMBA KWA MKOPO WANGEWEKA ANGALAU M40!
kAMA UNACSH NYUMBA ZILE UNAWEZA KUJENGA KWA ELF KUMI
 
Mfuko wa Pensheni wa PSPF unapenda kuutaarifu Umma kuwa umezindua Mpango Mpya wa uuzaji nyumba zake zilizojengwa kwa ajili ya makazi katika mikoa ya Dar es Salaam- Ilala (Buyuni), Morogoro (Lukobe), Tabora (Usule), Mtwara (Mang'amba), Shinyanga (Ibadakuli) na Iringa (Mawelewele).

Bei za nyumba ni kati ya sh. 52,000,000.00 hadi sh. 71,000,000.00 (bila VAT). Bei hizi ni kulingana na ukubwa wa nyumba na mkoa nyumba ilipo. Ukubwa wa nyumba ni kuanzia vyumba viwili hadi vinne.

Chini ya utaratibu huu mpya unaoanza kutumika kuanzia Februari 2014; Muombaji atapaswa kuainisha kwenye fomu ya maombi aina ya nyumba anayohitaji na Mkoa ilipo. Malipo yanaweza kufanyika kwa njia zifuatazo:

1) UNUNUZI KAMA MPANGAJI (HIRE PURCHASE):
Mnunuzi atalipia kwa mpango wa mwezi mmoja mmoja au miezi mitatu kwa mkupuo (installments) kulingana na thamani ya nyumba. Katika mpango huu, mnunuzi anaweza kulipia kutokana na vyanzo vingine vya mapato yake mbali na mshahara wake. Mwanachama wa PSPF aliyechangia chini ya miaka mitano (5) atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 5,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba na asiye mwanachama wa PSPF atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 10,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba kukidhi vigezo vya kununua nyumba (kama mpangaji).

Mpango huu wa Ununuzi kama Mpangaji (Hire Purchase) utamwezesha mnunuzi kulipa kati ya sh. 450, 000.00 (laki nne na hamsini tu) na sh. 813,000.00 (laki nane na kumi na tatu tu) kwa mwezi kama malipo ya nyumba zinazouzwa na Mfuko kulingana na ukubwa na eneo nyumba ilipo.

2) MALIPO YA MARA MOJA (OUTRIGHT PURCHASE)
Mnunuzi atalipia gharama ya kununua nyumba kupitia akaunti ya Mfuko na kisha kusaini makubaliano kabla ya kuhamishiwa umiliki (transfer).

3) MKOPO WA NYUMBA KUPITIA BENKI (MORTGAGE BASIS):
Mnunuzi anaweza kuchukua mkopo katika mojawapo ya Benki ambazo Mfuko wa PSPF ina mikataba nazo na kutumia mkopo huo kununulia nyumba. Mabenki hayo ni; CRDB, Azania, Exim na NMB.

MUHIMU! Iwapo utanunua nyumba kupitia mkopo wa benki (Mortgage) utapaswa kuwa umesajiliwa kwenye Mfuko na kuchangia kwa muda wa miaka mitano au zaidi. Muda wa kurejesha mkopo ni mpaka miaka ishirini na mitano (25) kulingana na matakwa ya Benki husika.

Mwombaji anayehitaji kuona au kukagua nyumba awasiliane nasi kupitia simu: +255 22 2120912/52 au +25522 2127375-6 au E-mail: pspf@pspf-tz.org.
Kwa maelezo zaidi fika Makao Makuu ya PSPF yaliyopo jengo la Golden Jubilee Towers, Barabara ya Ohio au ofisi zetu zilizopo katika kila mkoa.
Imetolewa na

Mkurugenzi Mkuu,

Mfuko wa Pensheni wa PSPF

Tunaomba pia mobile number kama ipo ndugu yangu. Ahsante sana
 
vijumba vyenyewe vibaya nilibahatika kuvihona vile vibanda sio nyumba za chanika buyuni ni bora za nhc kigamboni bei nafuu
 
Mbona hazilingani na bei iliyotajwa??? Zilitakiwa ziwe around 30M au 40M kwa mahesabu ya haraka
 
52 mil siyo pesa ndogo hata kidogo,labda wafanyabiashara wakubwa na watumishi wa ngazi za juu,walimu wote wapo pspf but sidhan kama kuna atakayethubutu hapo hata university lecturer.
 
Mwenye mbwa.....
Nimeona kuna minazi, nayo inauzwa kivyakevyake au pamoja na nyumba.... Usicho maswali maadamu umejitolea kuwa wakala wa pspf

we una taka kuona tangazo toka kwa mwenye mbwa ama mbwa mwenyewe hahahahaha
mimi nimelikuta huko mitaani na kulileta hapa,maana wenye mapasi pia wamo humu JF,kwa hiyo mnaweza jipatia nyumba hizo bila shaka
 
52 mil siyo pesa ndogo hata kidogo,labda wafanyabiashara wakubwa na watumishi wa ngazi za juu,walimu wote wapo pspf but sidhan kama kuna atakayethubutu hapo hata university lecturer.

ni gharama kwa kweli
ndio maana mama wenye nyumba huwa wanakuwa mbogo kweli kwa wapangaji wao
 
Mimi bado kabisa sijaweza kupiga hesabu vizuri ili niweze kuziita hizi nyumba "Za gharama nafuu"
 
ni gharama kwa kweli
ndio maana mama wenye nyumba huwa wanakuwa mbogo kweli kwa wapangaji wao

mimi nimefanikiwa kwenda kuziangalia,kiukweli siyo mbaya sana hasa
ukizingatia gharama za ujenzi siku hizi zipo juu sana,hlf hiyo picha
hapo juu ni ya nyumba ya vyumba viwili ila zipo za vyumba 3 na
vi4,gharama yake siyo mbaya sana hasa ukinunua kwa njia ya kukopeshwa
kama mpangaji.pia hizo nyumba zimekamilika kila kitu,sasa hivi wapo katika hatua ya kuzivutia maji na umeme.
 
Bei wanayouza ni mara mbili zaidi ya bei ya ujenzi wa hizo nyumba(Kiwanja, ujenzi wa nyumba yenyewe, maji na umeme)
 
hii wanunue wenye vijipesa vya ugoro, kwa sisi wa vijisenti hatuwezi
 
Back
Top Bottom