Visa gani!Tanzania tuna visa sana, sisi hatuna madaktari lakini wale tulio nao ndiyo hao wamebandikiwa tangazo waende zao Kenya.
Kila siku tunaambiwa serikali ina hela, na haiajiri kwakua kuna kutafuta watumishi hewa.Visa gani!
Kama serikali haina uwezo wa kuwaajiri unataka wakafanye kazi huko serikalini bure? Ok, tuseme wasiende..kuwepo hapa nchini kutaisaidia nini nchi wakati hawafanyi kazi ya taaluma yao?
Nendeni madaktari nendeni...Muhimu kama kipato kinaridhisha na usalama unaruhusu.
"Za kuambiwa changanya na zako" Kamata fursa kwanza...kula miaka miwili Kenya hawa wanaohakiki watakuwa wanamalizia uhakiki wao.Kila siku tunaambiwa serikali ina hela, na haiajiri kwakua kuna kutafuta watumishi hewa.
Siku wakishamaliza swala la watumishi hewa watawarudisha hawa nyumbani?