Tangazo la ajira Jeshi la Polisi 2014/2015

Tangazo la ajira Jeshi la Polisi 2014/2015

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Ajira kwa Wahitimu Elimu ya Juu Mwaka 2014
Katika mwaka wa fedha 2014/2015 Jeshi la Polisi Tanzania linatarajia kuajiri wahitimu wa vyuo vya Elimu ya Juu wa mwaka 2013/2014. Ili kutekeleza azma hii waombaji watajaza kikamilifu na wataambatanisha vivuli vya vyeti vyao na kutuma Makao Makuu ya Polisi kwa njia ya Posta kabla ya tarehe 31.08.2014 kwa anuani ifuatayo.

Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S. L. P. 9141,
DAR ES SALAAM

Waombaji wawe na taaluma zifuatazo:

Shahada: Menejimenti ya Rasilimali Watu, Utawala katika Utumishi wa Umma, Uchumi, Saikolojia na Ushauri Nasihi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji[BaLE], Sheria, Ualimu, Maendeleo ya Jamii, Uandishi wa Habari, Uandishi wa Habari za Michezo, Mawasiliano ya Umma, TV & Redio Production, Michezo, Ugavi[BA in Procurement & Supplies], Mawasiliano ya Redio[Bsc in Radio Communication], Mazingira[BA in Environmental Disaster Mgt], Uhandisi Mitambo, Uhandisi Madini[Mining Engineering], Uchoraji[BA in Fine Arts], Fedha na Benki[Finance & Banking], Daktari[Medical Doctor] na Daktari wa Meno[Dental Surgeon], Mkemia, Bailojia[Molecular Biology].

Stashahada: Utunzaji Kumbukumbu, Katibu Muhutasi[Personal Secretaries], Mawasiliano ya Redio, Matengenezo ya Kompyuta, Fax na Photocopy Machines, Mafundi Mitambo wa Meli, Mafundi Umeme wa Magari, Ugavi[Procurement & Supplies], TV na Video Production, Manahodha, Tabibu[Clinical Officer], Tabibu wa Meno[Dental Therapist], Mzoeza Viungo[Psysiotherapist/Occupational Therapist], Fundi Sanifu Mionzi[Radiographer] na Fundi Sanifu Macho[Optometrist].

Astashahada: Uzamiaji, Mpishi, Fundi Pikipiki, Fundi Ushonaji na Muuguzi Msaidizi[Enrolled Nurse].

MASHARTI KWA MWOMBAJI
1. Mwombaji atajaza fomu ya maombi kikamilifu na atabandika
picha yake "Ppt Size" kwenye fomu.
2. Mwombaji aambatanishe katika fomu vivuli vya vyeti vyote
yaani cheti cha kuzaliwa, kuhitimu elimu ya sekondari[Leaving
& Academic], cheti/vyeti vya taaluma[Academic Transcript].
3. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

SIFA ZA MWOMBAJI
1. Awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
2. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25.
3. Awe amehitimu chuo mwaka wa masomo 2013/2014 tu.
4. Awe na tabia njema.
5. Asiwe na kumbukumbu za kutenda uhalifu.
6. Awe na afya njema[kimwili na kiakili]
7. Awe hajaoa/hajaolewa au kuwa na mtoto.
8. Asiwe na alama za kuchora mwilini[tatuu].
9. Awe na urefu usiopungua sentimita 155.
10. Asiwe mtumiaji wa madawa ya kulevya.
11. Awe hajaajiriwa na idara nyingine Serikalini.
12. Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Polisi.
13. Awe tayari kufanya kazi popote ndani na nje.
fomu ya ajira elimu ya juu (1).pdf


 
Kuna maeneo hawatapata watu ng'oo........
 
polisi inaonekana wanataka watoto sana ofisini mwao..
 
Huu msalo tena. Nikiediti vyeti cpelekwi srgerea kweli. Nina masika 26
 
polisi inaonekana wanataka watoto sana ofisini mwao..

mkuu lazima uende lindo kwanza hata kama una degree then ndo upendekezwe kwenda kuchukua nyota kurasini after three years.

vijana fursa hizo
 
nafikiri ili tangazo limetoka tu, maana nadhani watafuatwa J.KT na walikuwa wanasubiri.
 
usaili wa Jkt tayari na walioko depo moshi CCP wanamaliza mwezi ujao baada ya kozi ya miezi karibia kumi sasa ni usaili wa form four na six then diploma and graduates.

all in all best wishes vijana hasa police professional BALE huu ndo wakati wa kuonesha ulichojifunza kwa miaka mitatu
 
shahada harafu miaka 25 waongeze kidogo

mkuu embu jaribu kwenda kwenye website ya polisi ili uwe na uhakika zaidi, maana hata mwaka jana umri ulikuwa miaka 18-25 ila kwa diploma na wenye vyeti ila kwa degree ni miaka18-28. OVER
 
Hii nchi wizi mtupu!!mtoto wa muuza gongo akiwa polisi sawa.ila hizo nafas mkipeana wakubwa sisawa ila poa tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom