Tangazo kwa madaktari wa Tanzania kwenda kufanya kazi Kenya

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
*JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA*
*WIZARA YA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WAZEE NA WATOTO*

*TANGAZO LA KAZI KWA MADAKTARI*

WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII ,JINSIA WAZEE NA WATOTO WANAPENDA KUWAARIFU WANANCHI KUWA *SERIKALI YA KENYA* INA MAFASI 500 ZA AJIRA ZA MKATABA KWA MADAKTARI WATANZANIA WENYE SIFA AMBAO WANGEPENDA KUFANYA KAZI NCHINI KENYA WATUME MAOMBI YAO KWA NJIA YA BARUA PEPE AMBAYO NI maombiyakazi@moh.go.tz KABLA YA *TAREHE 27 MACHI SAA 10:00 JIONI* BAADA YA HAPO MAOMBI HAYATAPOKELEWA
MAOMBI YAAMBATANISHWE NA NYARAKA ZIFUATAZO

1.WASIFU (CV) YA MWOMBAJI
2.NAKALA ZA VYETI VYA TAALUMA
3. TRANSCRIPT
4 NAKALA YA CHETI CHA KUZALIWA
5.CHETI CHA KUHITIMU INTERNSHIP
6.NAKALA YA CHETI CHA USAJILI KUTOKA BARAZA LA MADAKTARI LA TANGANYIKA

NB: *PAMOJA NA NYARAKA ZILIZOTAJWA HAPO JUU ,MUOMBAJI ANATAKIWA KUJAZA JEDWALI LILILOAMBATANISHWA NA TANGAZO HILI KATIKA MFUMO WA EXCEL*

*TANGAZO HILI HALIWAHUSU* WATUMISHI WA UMMA ,HOSPITALI TEULE ZA HALMASHAURI NA HOSPTALI ZA MASHIRIKA YA HIARI AMBAO WANALIPWA MSHAHARA NA SERIKALI.

WATAKAOKIDHI VIGEZO NA SIFA WANATARAJIWA KUPEWA MKATABA WA AJIRA MIAKA MIWILI(2)

*IMETOLEWA NA:*
Katibu Mkuu (Afya)
Wizara Ya Afya ,Maendeleo Ya Jamii ,Jinsia Wazee Na Watoto
DODOMA
18 MACHI,2017
1489831137381.jpg
 
Daaa tangazo limeandikwa kichekechea chekea anyway wenye sifa watakuwa wamesikia bila Shaka
 
Sijui kwanini kenya wanapenda kutujaribu na kutufanya wajinga?
 
Tanzania ni serikali ya kijinga sana imekalia kupeleka madaktari Kenya wakati sisi tuna uhaba wa madaktari serikali ya pombe hii
 
Mawazo ya wanasiasa bwana ni ya kipumbavu sana.....

Madaktari si walishakataa... Labda wangeimba madaktari wa jeshini?
 
Mawazo ya wanasiasa bwana ni ya kipumbavu sana.....

Madaktari si walishakataa... Labda wangeimba madaktari wa jeshini?
Kuna mwenye kukataa Mbele ya mkulu!? Wataalam walikataa ila yeye mwanasiasa kukwepa zigo la ajira amekubali, yote iyo ni kutaka kujinadi kua kawatafutia ajira tena anawaita "madaktari wangu" hahahaha, ila wajiangalie sana huko waendako Kenya sio kama bongo wao si watu wa maneno maneno meengi ni vitendo tu
 
Hahaah mmeshindwa kuwaajiri...eti mnapeleka kenya madaktari wakati tanzania kwenyewe hawatoshi...wapeni msaada bhc na wawalimu wa science
 
Back
Top Bottom