Tanga kunani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanga kunani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chimunguru, Jul 4, 2011.

 1. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Wadau! hasa wale ndugu zangu wa TANGA hebu nihabarisheni, Tanga driving school bado ipo? jumba la sinema likiitwa Tanga Majestic Cinema bado lipo? sababu ya kuuliza ni kwamba kuna ndugu yetu tulikuwa tunaishi naye Sumbawanga miaka ya themanini mzazi wangu alimpeleka Tanga kusomea udereva huko Tanga miezi mitatu, aliporudi kwa kweli aliusifia saaana mji wa Tanga na hasa hapo majestic cinema walikuwa wanatoroka hapo chuoni kwenda kuangalia picha. Kwa kweli hizo sifa zilistick kichwani mpaka leo naota nifike Tanga sababu sijawahi fika huko. alisifia saana barabara za Tanga.Hiyo Majestic ilimlostisha hakuweza kuwa dereva mzuri sababu kuna siku mshua alikuwa anaoga kasahau funguo sebuleni jamaa akazinyaka wakati ule no automatic tena mandolini pick up, jamaa akawasha akaingiza namba moja cruch akaiachia haraka gari ikaruka akapanic akakanyaga mafuta tena kwa nguvu next stop ni kwenye mahindi akalisweka hukooo wee ilikuwa soo wote tulichezea kichapo.Tanga waja leo warudi leo
   
 2. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  mwenzio mbona unanitisha mbona nataka kwenda Tanga,ila staki kurudi siku hiyohiyo ushauri mkuu.
   
 3. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  ni kuzuri istoshe, ................ labda kama una lako jambo maana waswahili nyie hamtabiriki.
   
 4. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  maana ya waja leo waondoka leo ni kwamba, ukifika tanga, ukakumbana na mwanamke akakupeleka kwake basi hautatoka siku hiyo hiyo.
  ukitaka kuondoka utamsikia mwanamke anakubeleza " jamani waja leo wandoka leo?" hapo kumbuka suruali imeshalowekwa kwenye maji.kwahiyo lazima ughairishe safari ya kurudi ulipotoka.
   
 5. KUNANI PALE TGA

  KUNANI PALE TGA Senior Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Chimunguru,Wakati ule Tanga kweli ilikuwa ni sehemu ambapo watu wengi walifika kwa ajili ya kupata likizo,kwa sababu kulikuwa na social activities nyingi sana,kutoka nyumba za sinema,parks,michezo na kadhalaika.But now my friend tanga is one of the dead cities in Tanzania.Hakuna kitu,majumba yote ya sinema zimekufa,viwanda zote zimekufa,barabra katikati ya mji ni ya kuaibisha.Hii yote ni siasa mbovu with a i dont care type of government.Watu ambao walihama Tanga miaka hiyo,na wakirudi sasa kwa ajili ya kutembelea ndugu,machozi yanawatoka kwa kuangalia hali mbaya ya mji wa Tanga,na watu wake walivyochoka kimaisha.Umaskini ni wakutisha,kazi hamna kabisa,vijana wameishia kuvuta bangi na kwenye madawa ya kulevya.Once it was the best place in tanzania,but now its like a ghost town.
  May god bless Tanga,so as it gets it glory best by this country to get a honest,caring,leaders.
  Asante.
   
Loading...