TANESCO yapeleka maombi EWURA kuomba kupandisha bei ya umeme

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Shirika la Umeme (Tanesco) limepeleka maombi kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), kuomba kupandisha bei ya nishati hiyo, kinyume na matakwa ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ya kushusha bei hiyo.

Taarifa ya Ewura kwa umma iliyotolewa kwenye vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa maombi hayo yamepokewa Jumatano ya wiki hii na kutaka wadau kujitokeza kujadili uhalali wa nyongeza hiyo siku mkutano huo utakapoitishwa.

“Mamlaka inaanzisha mchakato wa kupata maoni ya wadau, ili kujua uhalali wa maombi ya nyongeza ya bei za huduma iliyoyapokea kutoka Tanesco,” imeeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Tanesco iliwasilisha ombi husika kulingana na Sheria ya Umeme namba 131, inayoitaka Ewura kufanya mabadiliko ya bei zinazotozwa na mtoa huduma mara moja kila baada ya miaka mitatu.

“Pendekezo la wastani wa badiliko la bei za umeme ni asilimia 1.1 kuanzia Aprili mosi 2016 na asilimia 7.9 kuanzia Januari mosi 2017,” limeeleza tangazo hilo.

Mapendekezo hayo japo ya kisheria, lakini yanapingana na msimamo wa Waziri Muhongo, ambaye tangu alipoapishwa kushika wadhifa huo, alielezea kusudio lake la kutaka bei ya nishati hiyo ishushwe.

Profesa Muhongo alikwenda mbali na kuagiza Tanesco, Ewura na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), kumpelekea mapendekezo ya kushuka kwa bei ya umeme kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu.

Katika maagizo hayo, Profesa Muhongo alihoji kwa nini bei ya umeme isishuke, wakati gharama za uzalishaji wa umeme wa kutumia mafuta zimeshuka kutokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

Kutokana na maombi hayo ya Tanesco, Ewura imewataka wadau wa nishati wanaopenda kutoa maoni yao kwa maandishi, kufanya hivyo kwa kutuma maoni yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, ghorofa ya saba jengo la LAPF Pensions Fund Tower, mkabala na Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama Dar es Salaam.

Kwa watakaotuma kwa njia ya posta, wameombwa kufanya hivyo kwa kutumia Sanduku la Posta 72175, Dar es Salaam, Tanzania, simu namba (+255-22) 2123853-4; Fax namba (+255-22) 2123180; Barua pepe info@energyregulators.org au tovuti Hébergement Internet, Cloud, et Serveurs dédiés - OVH. energyregulators. org.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mamlaka hiyo pia, itaitisha mikutano ya wazi ili kukusanya maoni kuhusu mapendekezo hayo kutoka kwa wadau mbalimbali, wakiwamo Baraza la Wawakilishi wa Watumiaji wa Huduma (CCC); Baraza la Ushauri la Serikali (GCC) pamoja na wananchi kwa ujumla.

Chanzo: Mpekuzi Blog
 
Kuna wakati mwingine mtu anaweza kukuomba utoe maoni juu ya jambo fulani ukaishia kumtukana matusi ya nguoni, mtu unawaza upumbavu afu unaomba watu watoe maoni juu ya upumbavu uliowaza. Hawa Tanesco siimani kabisa kama raisi wetu hadi leo hajagundua kua ni jipu kuu, kwanza jinsi inavyoendeshwa, unawezaje kuagiza nguzo south africa wakati south afrika wao wananunua nguzo Iringa. Pumbavu kabisa huyo anayeomba kuongeza bei ya umeme.
 
Haaa, KUONGEZA? wakati bei ya mafuta imeshuka , maji nayo mafuriko kila kona nchi hii, gesi ndio hiyoooo kila siku inagunddulika, kwa nini hawa viongozi hawa jiongezi? Hii nchi ina laana si bure.
 
SHIRIKA la Umeme (Tanesco) limepeleka maombi kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), kuomba kupandisha bei ya nishati hiyo, kinyume na matakwa ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ya kushusha bei hiyo.
Taarifa ya Ewura kwa umma iliyotolewa kwenye vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa maombi hayo yamepokewa Jumatano ya wiki hii na kutaka wadau kujitokeza kujadili uhalali wa nyongeza hiyo siku mkutano huo utakapoitishwa.
“Mamlaka inaanzisha mchakato wa kupata maoni ya wadau, ili kujua uhalali wa maombi ya nyongeza ya bei za huduma iliyoyapokea kutoka Tanesco,” imeeleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Tanesco iliwasilisha ombi husika kulingana na Sheria ya Umeme namba 131, inayoitaka Ewura kufanya mabadiliko ya bei zinazotozwa na mtoa huduma mara moja kila baada ya miaka mitatu.
“Pendekezo la wastani wa badiliko la bei za umeme ni asilimia 1.1 kuanzia Aprili mosi 2016 na asilimia 7.9 kuanzia Januari mosi 2017,” limeeleza tangazo hilo.
Mapendekezo hayo japo ya kisheria, lakini yanapingana na msimamo wa Waziri Muhongo, ambaye tangu alipoapishwa kushika wadhifa huo, alielezea kusudio lake la kutaka bei ya nishati hiyo ishushwe.
Profesa Muhongo alikwenda mbali na kuagiza Tanesco, Ewura na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), kumpelekea mapendekezo ya kushuka kwa bei ya umeme kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu.
Katika maagizo hayo, Profesa Muhongo alihoji kwa nini bei ya umeme isishuke, wakati gharama za uzalishaji wa umeme wa kutumia mafuta zimeshuka kutokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.
Kutokana na maombi hayo ya Tanesco, Ewura imewataka wadau wa nishati wanaopenda kutoa maoni yao kwa maandishi, kufanya hivyo kwa kutuma maoni yao kwa Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, ghorofa ya saba jengo la LAPF Pensions Fund Tower, mkabala na Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama Dar es Salaam.
Kwa watakaotuma kwa njia ya posta, wameombwa kufanya hivyo kwa kutumia Sanduku la Posta 72175, Dar es Salaam, Tanzania, simu namba (+255-22) 2123853-4; Fax namba (+255-22) 2123180; Barua pepe energyregulators. org.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mamlaka hiyo pia, itaitisha mikutano ya wazi ili kukusanya maoni kuhusu mapendekezo hayo kutoka kwa wadau mbalimbali, wakiwamo Baraza la Wawakilishi wa Watumiaji wa Huduma (CCC); Baraza la Ushauri la Serikali (GCC) pamoja na wananchi kwa ujumla.
SOURCE: www.darwaya.com
 
Mimi siamini kama viongozi wa nchi hii wana akili timamu, siamini hilo kabisaaa.

Yaani kuhusu kupandisha bei ya umeme nikatoe maoni?

Hawa watu ni vichaa
 
...hili jipu sijui litatumbuliwa lini,au limejificha halionekani? labda lipo kwenye utumbo.!!
 
Hii nchi bhana!! Kila siku kituko, maana tuliambiwa bunge la Makinda kwamba umeme utashuka bei, waziri Muhongo kaagiza bei ya umeme ushushwe, na tukasikia toka Tanesco wenyewe kwamba wamesha mpelekea waziri mapendekezo ya kushusha bei ya umeme, leo hao hao wanaomba kupandisha bei?????? Hivi kuna nini huko Tanesco. Ati bei ya mali ghafi, hii ni aibu, maana tayari wanatumia gas, bei ya mafuta ghafi imepungua kwa kiasi kikubwa lakini wao wanasema imeongezeka.
Bunge limepiga kelele na IPTL serikali sikivu ya Ccm imekaa kimya haisikii mzigo wa Tanesco tuwabebe sisi Walala hoi wao wale bata. Naona tufike mahali tuseme kwa sauti kubwa sasa Tanesco baaaassssiiiiii
 
Mmmh...mbona wanatuzingua...mara wanashusha mara wanapandisha...halafu yule "Muongo" anasema wanataka wauze umeme na gesi nje...hii nchi ni sawa na baba anayeuza chakula na kuwaacha watoto wakimbwelambwela kwa mabaki...
 
image.jpeg

Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), limewasilisha kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), maombi ya kupandisha bei ya huduma ya Umeme nchini kuanzia Aprili mosi mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa zilizowekwa kwenye tovuiti ya EWURA, TANESCO wamewasilisha maombi hayo kwa mujibu wa Sheria ya Umeme namba 131, inayoitaka EWURA kufanya mabadiliko ya bei zinazotozwa na mtoa huduma mara moja kila baada ya miaka mitatu.TANESCO wanataka kupandisha bei kwa asilimia 1.1 mwezi Aprili na kufikia 7.9 ifikapo Januari 2017.

Hali hii inatokea na kupingana na kauli ya Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo,ambaye hivi karibuni amenukuliwa akisema ameshawaagiza EWURA,TANESCO na TPDC kufikia mwezi wa saba wawe wameshirikiana kuhakikisha kuwa bei ya umeme inashuka kwa kiasi kikubwa.Hii hali ya kupandishiwa bei ya umeme inazidi kutuchanganya sisi raia,maana tuliambiwa gesi ya Mtwara itapunguza bei ya upatikanaji wa umeme na kupunguza kabisa kitu inayoitwa mgao wa umeme.

Waziri wa Nishati na Madini wakati huo Simbachawene,aliliambia Bunge kuwa ifikapo 14/09/2015 tatizo la umeme na kupanda kwa bei litakuwa limekwisha sbb mradi wa gas wa Kinyerezi utakuwa umekwisha na kuanza kazi,lakini leo kuelekea mwezi March hali ya umeme bado ni tete na bei ni juu.Jamani hivi tutadanganyana mpaka lini.
 
Back
Top Bottom