Tanesco yaingiza nchini mita za Luku 11,000 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco yaingiza nchini mita za Luku 11,000

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 21, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Luku


  Hatimaye Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), limeanza kuingiza mita za Luku ambazo jana zilianza kusambazwa katika mikoa mbalimbali.

  Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Adrian Sererin, aliliambia NIPASHE jana kuwa hadi sasa mita 11, 500 zimeishaingizwa nchini.

  Aidha, alisema Mita zingine 75, 000 zinatarajia kuingizwa nchini ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafungiwa kwa nchi nzima.

  Kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu, Tanesco lilikuwa linakabiliwa na uhaba wa ,ita na vifaa vingine ambavyo vinahitajika kwa ajili ya kuwaunganishia wateja umeme.

  “Hivi sasa hatuna tena uhaba wa mita na tumeishaingiza mita za kutosha na jana (juzi) tulianza kuzisambaza mikoani ili zianze kufungwa kwa wateja,” alisema.

  Alifafanua kuwa Tanesco inatarajia kufunga mita mpya kwa wateja wote na kuondoa zile za zamani na kwamba zoezi hilo linatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi ujao.

  “Hizi Mita zote za sasa zitabadilishwa na kuweka mpya kwa nchi nzima na hivi tunavyoongea tayari zimeanza kusambazwa mikoani,” alisema Zaidi ya wateja 6000 walioomba kuwekewa umeme katika maeneo mbalimbali wameshindwa kupata huduma hiyo kutokana na Tanesco kutokuwa na mita kwa kipindi kirefu.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kinachoniuma mimi ni hizo mita zingeweza kutengenezwa nchini tena nawatanzania! Badala yake bado tutaendelea kuingiza vitu kutoka nje ya nchi sijui hadi lini maana sioni mikakati ya maana kuhusu kupunguza uagizaji wa vitu vya umeme kutoka ng'ambo!!
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Hizo mita za luku mutengeneze wenyewe na hao Mafisadi watakula wwapi?
   
 4. s

  sanjo JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kimkakati TANESCO ni shirika linalojiendesha kwa kama idara ya moto (Fire Brigade Operation Department). Wanasubiri umeme ukatike ndio waanze kutafuta sababu ya kukatika. Mara maji ysa Mtera na Ruaha yamepungua, mara serikali haijawekeza miundo mbinu kwa miaka mingi nk. Mambo hovyo hovyo kabisa.
   
 5. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Katika mashirika yanawapa kiburi wanasiasa ni hili mojawapo, linakera sana! mbaya zaidi wafanyakazi hawajui wananguvu kiasi gani kuwastopisha hawa waheshimiwa wasiendelee kusumbua. Wanavitengo vingi, utakuta kitengo cha utafiti makao makuu, kitengo cha miradi endelevu makao makuu, kitengo cha Training makao makuu kazi yao ni kujilipa posho na kuandika report ambazo sijui kama wanazisoma na kuwasaidia.
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kelele za kunguru hazimzuii kuku kula chakula chake wewe itabidi ungojee mwaka 2015 umpe kura yule unayemuona anafaa

  kukuongoza. Malalamiko yako au yetu hayasidii kitu Mafisadi wanakula na kulala mahali pazuri, wewe mlala hoi ndio unaye teseka kwa hayo matatizo subiri umchague yule unayemuona kuwa anafaa kuwa kiongozi wako tu.
   
 7. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ni mchakato mrefu mkuu!! Ni zaidi ya kumchagua kiongozi anayefaa! We need a clear distinction between the boundaries of country interests and politics. Wakati wa maslahi ya kitaifa, si chama chochote cha siasa chenye uwezo wa kuwa juu (na haki) ya kufanya pekee.
   
Loading...