Tanesco wanapolipiga changa la macho bunge letu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco wanapolipiga changa la macho bunge letu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NasDaz, Aug 26, 2011.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Kwa jinsi ilivyo inaonesha wazi kwamba serikali kwa kushirikiana na TANESCO wamekuwa wakiuhadaa umma kuhusiana na suala zima la upatikanaji wa umeme. Mbaya zaidi, hivi sasa hadaa hizi zinafanywa dhidi ya bunge.

  Wakati wa kampeni za uchaguzi 2010, hakukuwa na tatizo lolote la umeme, lakini mara mgao wa kutisha ukaanza mara baada ya uchaguzi huo. Tukaelewa; kwamba waliogopa kura za hasira endapo kungekuwa na umeme.

  Kwa bahati mbaya, wananchi hatuna pa kwenda, mgao huu wa kutisha ukaendelea hadi siku kabla ya bajeti ya wizara ya nishati na madini kujadiliwa kwa mara ya pili. Bila shaka, serikali tena kwa kushirikiana na TANESCO safari hii wakaamua kuwapiga changa la macho wabunge.

  TANESCO, wakatumia hadi tone lao la mwisho kuwahadaa wabunge kwamba umeme si janga tena. Bila kufahamu, wabunge wetu wakapitisha bajeti ya wizara ya nishati na madini huku wakiamini kwamba tatizo la umeme limepungua.

  Mara baada ya bajeti hiyo kupita, tatizo la umeme limerudi kama awali. Je, wabunge wetu nao wanakubali kuchezewa akili kiasi hiki na serikali kwa kushirikiana na TANESCO?

  Ili kuheshimu na kulinda hadhi ya bunge; ni kwanini bunge lisiwaite TANESCO na kuwakaripia kwa kuwachezea akili? NINGEKUWA mbunge, ningejisikia aibu kuchezewa akili kiasi hiki.

   
 2. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,068
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Bado najiuliza Makinda alitumia busara gani kuzuia hoja binafsi ya Wenje kuhusu nchi kuendelea kuwa gizani zaidi kuliko hata kabla bajeti ya wizara ya Nishati na Madini haijapitishwa.

  Naamini kama Makinda angekubali hoja hiyo bunge lingeweka wazi uongo wa Ngeleja nakumuwajibisha ipasavyo.
   
Loading...