TANESCO wakubali kubomoa jengo lao, waahidi upatikanaji wa umeme wakati wa kutekeleza agizo hilo

Jumlisha na pesa ya kubomolea hapo, alafu hilo jengo kwa sasa thamani yake ni zaidi ya bilioni 20

Thamani ya makisio ya 1998 ilikuwa billion 51 km sijakosea, Air condition iliyopo juu ya jengo inadhamani ya km billion 1.5 estimation
 
Thamani ya makisio ya 1998 ilikuwa billion 51 km sijakosea, Air condition iliyopo juu ya jengo inadhamani ya km billion 1.5 estimation
Hatari ndugu hilo jengo halina tofali aisee ni nondo za hatari na zege kali chini mpaka juu
 
Hili jengo likivunjwa narudisha cheti changu UDSM.Huu ni upumbavu na kamwe siwezi kukubaliana nao.
 
Wangelikwepa mngesema mbona Kimara wakazi hawakuwakwepa, hamkosi jambo nyie.

Maana halisi ya uongozi ni pamoja na kutoa maamuzi km hayo, kimara na bomoa na tanesco sibomoi ,
JK alisema lisibomolewe, alitumia Hekima ndio lipo barabarani lakini tu divert
 
Baada ya agizo la Mheshimiwa kutaka jengo la TANESCO livunjwe, ni wakati sasa wa kufuatilia na kujua ni kampuni gani na kwa utaratibu gani kampuni husika itapewa tender maana sidhani jengo refu kama lile linaweza kuvunjwa na greda za Manispaa ya Jiji au Halmashauri.

Wacha tusubiri.
 
Libomolewe tu mbona sisi za kwetu tumebomoa kwa maumivi makubwa.!
Lakini kulikuwa na zuio la mahakama. Na kwa vile kesi bado iko mahakamani huwezi jua ushindi waweza kuwa kwenu na fidia ikalipwa. Hivyo sio sahihi kushabikia lile jengo kubomolewa kwa sababu zenu zilivunjwa, kufanya hivyo ni kuhalalisha kuwa kilichotendwa kwenu nacho kilikuwa sahihi
 
Umenena hapo juu, mahakama ndo chombo cha kutolea haki, bila kupepesa macho hii ishu ya libomolewe au lisibomolewe ikienda mahakamani, saa mbili na robo asubuhi judge atasema toa hiyo kitu iko ndani ya hifadhi ya barabara.
na uzuri kwenye hilo la road reserve halinaga figisu figisu kwa kuwa mita haiwezi kubadilishwa na kuwa centmeter
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom