TANESCO: Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Umeme Nchini

TANESCO

Official Account
Jul 12, 2014
4,584
2,104
SERIKALI kupitia TANESCO imefanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya umeme Nchini ambao haujawahi kutokea Katika Historia ya uwekezaji katika Sekta ya Umeme.

Miongoni mwa Miradi mikubwa ya umeme inayotekelezwa ni pamoja na upanuzi wa Kinyerezi I, ujenzi wa Kinyerezi II, Kinyerezi III, Kinyerezi IV, Malagarasi Mkoani Kigoma, Lusumo Falls Mkoani Kagera, Kikonge Mkoani Luvuma, Mkoani Mtwara na mingine mingi.

Kwa upande wa miradi ya ufuaji umeme, Sekta binafsi nayo haikuachwa nyuma katika harakati za ufuaji na usafirishaji umeme Nchini, Kwa kuzingatia kuwa azma ya Serikali ni kufikia ufuaji wa umeme wa Megawati 5,000 ifikapo 2020 na Megawati 10,000 ifikapo 2025. Kwa kuzingatia hilo Serikali ilianzisha mkakati maalum wa kuongeza uwekezaji katika miradi ya kuzalisha umeme ambayo inatekelezwa kwa kushirikiana na Sekta binafsi kutoka ndani na nje ya Nchi.

Sekta binafsi imeshirikishwa katika miradi midogo ya Nishati Jadidifu (Renewable Energy) yenye MW 16.29, imetekelezwa na Sekta binafsi, nayo ni Miradi midogo ya kuzalisha umeme wa maji (Min Hydropower) ambayo ni Uwemba- MW 0.84, Mwenga MW 4, na Yori MW 0.95, na Miradi midogo ya kuzalisha umeme kwa kutumia tungamo taka (Biomass) ni Tanwat MW 1.5 na TPC MW 9.0.

Aidha, Katika kuhakikisha kwamba Taifa linapata umeme wa uhakika, Serikali imeendelea kufanya jitihada mbali mbali za kuongeza na kuimarisha mtandao wa usafirishaji na usambazaji umeme, (National Grid) unaounganisha Nchi nzima kwa kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa njia za kusafirisha umeme kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika maeneo mengi ya nchi yetu.

Mradi wa kuunganisha Nchi za Tanzania – Uganda (Mwanza – Masaka 220 KV) ambao utaboresha hali ya umeme kwa Kanda ya Ziwa, Ujenzi wa njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovolti 400 kutoka Mkoani Iringa hadi Shinyanga, Mradi wa ujenzi wa njia kubwa ya umeme ya 400KV kutoka Singida - Arusha – Namanga, mradi huu utawezesha kuboresha kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa Mikoa ya Kaskazini.

Miradi mingine ni Mradi wa ujenzi wa njia ya 220 KV (Western spur.) utakaoanzia Tunduma, Sumbawanga, Kigoma mpaka Kyaka, mradi huu utaunganisha katika Gridi ya Taifa, Mikoa ya Songwe, Rukwa, Kigoma mpaka Kagera na hivyo kuboresha hali ya umeme katika kanda ya Magharibi, Mradi wa Chalinze hadi Arusha, Kanda ya Kaskazini (North West Grid), Mradi wa Njombe, Songea na Mbinga (South west Grid), mingine ni ya uzalishaji umeme ya Kinyerezi (Megawati 240), Luhudji (Megawati 400) na mingineyo, Uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam, City Centre-Dar es Salaam na Electricity V.

kutokana na uwekezaji huo mkubwa,na uboreshaji wa Miundombinu unaofanywa na TANESCO, hakutakuwa na upungufu wa umeme Nchini, Mwaka 2015 Nchi ilikuwa na upungufu wa umeme wa jumla ya Megawati 300, na maeneo mengine yalikuwa na hali mbaya hususan Mwanza, Arusha na Kilimanjaro lakini kwa sasa hali ya umeme katika Mikoa yote na mingine ni nzuri na hakuna upungufu wa umeme na kama ikitokea umeme umekatika ni matatizo ya kiufundi katika eneo dogo na kwa muda mfupi.

Sambamba na uwekezaji unaoendelea, TANESCO imeongeza juhudi za kusambaza umeme kwa Watanzania wengi zaidi kote Nchini, maeneo ya Mijini na Vijijini. Aidha, katika Takwimu mpya za kiwango cha utumiaji wa umeme Nchini zilizotangazwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ambazo zilizotayarishwa na Wakala wa Taifa wa Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na REA, TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini zinaonesha hadi kufikia Desemba 2016: (i) Watu wenye fursa ya kutumia umeme Nchini (Overall National Access Level) ni 67.5% (2007: ilikuwa 10%) ambapo Vijijini ni 49.5% (2007: ilikuwa 2%) na Mijini ni 97.3%.

Serikali kupitia TANESCO pia inaendelea kuhimiza Wananchi kuunganisha Huduma ya umeme katika maeneo yao ya Vijijini hii ni baada ya utekelezaji wa Miradi Kabambe ya REA kufanikiwa kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na kasi ya Wananchi ya kuunganisha Huduma ya umeme.

Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA TURNKEY PHASE III) ambao umeshaanza kutekelezwa. Mradi huu utatekelezwa kwa kipindi cha miaka 5 katika Vijiji 7,873 vya Wilaya zote za Tanzania Bara. Takribani Vijiji 7,697 vitapelekewa umeme wa Gridi ya Taifa na Vijiji 176 umeme wa nje ya Gridi (Off-grid).

Mpango huu utaongeza wigo wa usambazaji umeme katika maeneo ambayo hayakufikiwa na Mradi wa REA II (Turnkey Phase II)
 
Kwenye miuondombinu na umeme serikali imejitahidi sana. Lakini pia bado kuna ubabaishaji mwingi tu ambao unatakiwa kulekebishwa. Mwaka huu hatukuona mgao wa umeme kama ilivozoeleka kwa Tz.
Naibu waziri wa nishati na madini yule unafanya kazi vizuri sana.

Kwa kweli hadi leo bado namchukia sana
William Ngeleja. Huyu mtu alituharibia sana huyu asee.
 
Hongereni sanaa TANESCO,ila pia mngesaidia kupunguza bei ya unit za umeme ila hata wale wananchi wa hari ya chini waishio vijijini waweze kumudu gharama za kulipa bill ya umeme
wananua umeme unit moja kwa 500 tsh halafu wanauza kwa chini ya 300 halafu bado unataka wapunguze... kimsingi walitakiwa kupandisha ....
Nafikiri suluhu ni kutafuta suluhu ya kuondokana na kununua umeme na hiyo mikataba tuliyo ingia
 
Huo umeme wa IPP tumeshaambiwa ni ghali. Zungumzieni ya kwenu kama TANESCO badala ya kuimba ya sekta binafsi.
 
TANESCO mnafanya kazi nzuri sana lakini mngejipunguzia majukumu ili muweze kusimamia vyema sector hii. Kazi ya kusambaza umeme mngeachia sector binafsi. Pia umeme wa gesi haujaleta nafuu kwa watumiaji moja kwa moja sababu ya nyie kuuziwa ghali. ..kwanini tusiendelee kutumia umeme wa maji hadi tutapofikia muafaka wa bei ya gesi badala ya kuwatwisha zigo wananchi? Kama tukiwa na mkakati mzuri wa kutunza maji bado ni njia nafuu zaidi . Gesi bado haijaleta kile tulichotarajia ikiwemo hata gesi tunazouziwa mtaani bado ni ghali mno.
 
Sawa lakini kumbukeni Mkubwa na wanawe hawakubali hata kidogo na ndiyo maana akamwomba Waziri mkuu wa Ethiopia atumegee Watts kadhaa.

Nadhani mbereko yenu iko kwa Muhongo coz anauelewa mpana kwenye hiyo sector kuliko boss. Otherwise panga pangua kama ya bandarini ingewahusu. Inaelekea upande huu bado anahitaji kurudi UDSM ili akapate angalau ka diploma kwa mwezi 1, then ka bachellor mwaka 1, Mpaka 2019 atakuwa na PhD ya mambo ya huko so take care maana atawapelekesha Mpaka muombe pooo!
 
Hongera sana Tanesco kwa kazi kubwa mnayoifanya bila kujali ni holidays au muda gani. Kila siku mchana na usiku, nnyi na mafundi wenu mnakimbia hapa na pale kuhakikisha huduma zinaendelea kupatikana kwetu sisi wateja. Wakati mwingine hata wafanyakazi wenu wanapatwa na ajali na wengine kufariki, na yote hii ni ktk kuwahudumia wateja wenu. Lkn sisi wateja imekuwa ni kawaida yetu kulaumu na wengine wanaenda mbali zaidi kuzusha uongo Mradi wapate kuchafua kazi nzuri mnayofanya pasipokujali athari za upotoshaji wao.
Narudia kusema tena msikatishwe tamaa na wapinga Maendeleo ya Taifa hili.
 
Kimweri
Ndugu hakuna awamu ambayo haikukuta miradi ya awamu zilizopita. Alafu kuchafuana ipo kila awamu ...kama umri wako umesogea kidogo unakumbuka alivyoingia Mkapa? Lakini zaidi labda umesahau matusi ya Boyz I I Men kwa Mkapa na yale magazeti yao yaliyojaa makala za kusisimua tukaona tumepata majembe. ...awamu hii nayo itahukumiwa kwa wakati wake. ...kwasasa tuje na mawazo mbadala ya kujenga ....watusikilize wasitusikilize. ...ndio wajibu wetu kizalendo .....TANESCO wameleta taarifa yao. ...tuijadili. ..nategemea hoja nzito nzito kuwasaidia maana najua wewe ni miongoni mwa ma great thinker wa JF ...
 
Asante sana, tunapokea maoni na ushauri utakaotolewa, ili kuboresha ufanisi, utendaji na Huduma zetu kwa Jamii.
 
Hongera sana Tanesco kwa kazi kubwa mnayoifanya bila kujali ni holidays au muda gani. Kila siku mchana na usiku, nnyi na mafundi wenu mnakimbia hapa na pale kuhakikisha huduma zinaendelea kupatikana kwetu sisi wateja. Wakati mwingine hata wafanyakazi wenu wanapatwa na ajali na wengine kufariki, na yote hii ni ktk kuwahudumia wateja wenu. Lkn sisi wateja imekuwa ni kawaida yetu kulaumu na wengine wanaenda mbali zaidi kuzusha uongo Mradi wapate kuchafua kazi nzuri mnayofanya pasipokujali athari za upotoshaji wao.
Narudia kusema tena msikatishwe tamaa na wapinga Maendeleo ya Taifa hili.

Asante sana
 
Ndugu hakuna awamu ambayo haikukuta miradi ya awamu zilizopita. Alafu kuchafuana ipo kila awamu ...kama umri wako umesogea kidogo unakumbuka alivyoingia Mkapa? Lakini zaidi labda umesahau matusi ya Boyz I I Men kwa Mkapa na yale magazeti yao yaliyojaa makala za kusisimua tukaona tumepata majembe. ...awamu hii nayo itahukumiwa kwa wakati wake. ...kwasasa tuje na mawazo mbadala ya kujenga ....watusikilize wasitusikilize. ...ndio wajibu wetu kizalendo .....TANESCO wameleta taarifa yao. ...tuijadili. ..nategemea hoja nzito nzito kuwasaidia maana najua wewe ni miongoni mwa ma great thinker wa JF ...
Ulichosena sahihi kabisa. Yawezekana wao kunasibisha kuwa awamu hii ndio mzizi wa hii miradi kulinitubua na kuacha kuitazama taarifa yao objectively.

Natumai wasingeweka ile part ningeitazama kama taarifa., sasa naitazama kama Publicity stunt.
 
Kuanzia mwaka 1961 hadi sasa hatuna megawati 1400 pamoja na independent power producers (ukijumlisha wazalishaji binafsi kama aggreco, symbion, iptl, songas), miaka 3 hii iliyobaki kufikia 2020 hizo megawati 3600 zitatoka wapi ili kufikia megawati 5000?

Ukitoa kinyerezi 1,2 ambazo hazizalishi hata megawati 1000 ambazo labda tunategemea zitaanza kazi mwaka mmoja au miwili ijayo hzo nyingine zitatoka wapi?

Ni mradi gani ambao nategemea kutoa hizo mgawati karbu 3000 kwa miaka 2 ijayo ukitoa kiyerezi?

Tanesco acheni siasa.
 
Mnatumika na Serikali ili kuipigia debe!? Mbona matatizo chungu nzima ambayo yamesababisha TANESCO iwe na madeni ya zaidi ya bilioni 800 huyasemi?

Mbona kauli ya CAG kuhusu shirika kuendeshwa kwa hasara kubwa kutokana na kununua unit moja ya umeme kwa shilingi 544 na kuuza kwa wateja wenu kwa shilingi 279 unaikwepa!?

Nilidhani umeingia humu kuitetea TANESCO ili iboreshwe kwa manufaa ya Tanzania na Watanzania wa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo, kumbe unatumika kuipigia debe Serikali ambayo haistahili kupigiwa debe kuhusu lolote lile la TANESCO.

Msikilize CAG hapa kuhusu mojawapo ya matatizo ya TANESCO

Ukisoma Vizuri Mteja kunamiradi mingi, ambayo miongoni inasimamiwa na TANESCO
 
Mnatumika na Serikali ili kuipigia debe!? Mbona matatizo chungu nzima ambayo yamesababisha TANESCO iwe na madeni ya zaidi ya bilioni 800 huyasemi?

Mbona kauli ya CAG kuhusu shirika kuendeshwa kwa hasara kubwa kutokana na kununua unit moja ya umeme kwa shilingi 544 na kuuza kwa wateja wenu kwa shilingi 279 unaikwepa!?

Nilidhani umeingia humu kuitetea TANESCO ili iboreshwe kwa manufaa ya Tanzania na Watanzania wa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo, kumbe unatumika kuipigia debe Serikali ambayo haistahili kupigiwa debe kuhusu lolote lile la TANESCO.

Msikilize CAG hapa kuhusu mojawapo ya matatizo ya TANESCO

Asante sana Mteja kwa maoni, nia yetu ni kumfikia Mteja na kutatua changamoto zinazoeakabili wateja, ushauri na maoni ni namna gani tuboreshe utoaji wa Huduma.
 
Mnatumika na Serikali ili kuipigia debe!? Mbona matatizo chungu nzima ambayo yamesababisha TANESCO iwe na madeni ya zaidi ya bilioni 800 huyasemi?

Mbona kauli ya CAG kuhusu shirika kuendeshwa kwa hasara kubwa kutokana na kununua unit moja ya umeme kwa shilingi 544 na kuuza kwa wateja wenu kwa shilingi 279 unaikwepa!?

Nilidhani umeingia humu kuitetea TANESCO ili iboreshwe kwa manufaa ya Tanzania na Watanzania wa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo, kumbe unatumika kuipigia debe Serikali ambayo haistahili kupigiwa debe kuhusu lolote lile la TANESCO.

Msikilize CAG hapa kuhusu mojawapo ya matatizo ya TANESCO
Ukimsoma humo CAG Utakubaliana nami kuwa tatizo si tanesco bali tatizo ni mikataba na mahitaji ya watanzania..
Mikataba iliyosainiwa imesababisha tanesco waendelee kununua umeme kwa unit moja TSH500 halafu wauze chini ya 300... hapa suluhu ni kushauri jinsi ya kuvunja mikataba hii ya Tanesco na kushauri jinsi ya kulipa deni la tanesco ili tuweze kuinunua ile mitambo tuwe tunaiendesha wenyewe....
Tanesco wana jitahidi sana tena sana
 
Back
Top Bottom