Tanesco Moro wadai bilioni 8/-

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,081
JK iamuru hazina ilipe madeni ya taasisi mbali mbali za serikali yakiwemo mashule kwa TANESCO
Tanesco Moro wadai bilioni 8/-
Eline Shaidi, Morogoro
Daily News; Saturday,April 26, 2008 @00:05

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Morogoro, linadai kiasi cha Sh bilioni nane kutoka kwenye mashirika mbalimbali, ofisi za serikali pamoja na vyuo vilivyopo mkoani humo.

Akizungumza ofisini kwake, Meneja wa Tanesco mkoani hapa, Injinia Benglel Msofe alisema mbali na wadeni hao sugu, pia Tanesco inawadai fedha nyingi iliyokuwa Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC), fedha ambazo alidai kuwa zilitokana na baadhi ya viwanda kubinafsishwa na serikali bila ya kulipa bili za nyuma za umeme.

Alivitaja viwanda vinavyodaiwa na Tanesco kuwa ni Kilosa Cotton, Tanzania Sisal, pamoja na Afina Company, na kueleza kuwa hivi sasa hana idadi kamili ya fedha ambazo Tanesco zinadai PSRC. Alizitaja baadhi ya taasisi hizo kuwa ni Jeshi la Magereza, Polisi, Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania Kikosi cha Mzinga, na Pangawe.

Taasisi nyingine ni Chuo cha Ualimu Kigurunyembe, Shule ya Sekondari Mzumbe, pamoja na Tungi Estate na Hospitali ya Mkoa.

Msofe alisema hivi sasa shirika hilo lipo mbioni kukata umeme kwa wadaiwa hao kutokana na kuwaandikia barua ya kuwataka kulipa kodi zao kwa muda wa saa 48, kama ambavyo utaratibu wa shirika hilo hufuata kabla ya kukata huduma hiyo.

Shirika hilo hivi sasa limeanza zoezi la kukata umeme sehemu mbalimbali mkoani hapo kwa wateja ambao ni wadeni sugu, pamoja na wengine ambao wamekuwa wakilimbikiza madeni yao bila ya kulipa.

Meneja huyo aliyataja mashirika hayo kuhakikisha yanalipa bili zao kwa wakati na kuyataja mashirika ambayo yamekuwa yakilipa madeni kwa wakati kuwa ni Kilombero, D'Mond, Tumbaku, Vyuo Vikuu vya Sokoine (SUA), Mzumbe na cha Kiislamu, Kiwanda cha Nyama, benki pamoja na Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka (MORWASA).
 
Back
Top Bottom