KiuyaJibu
JF-Expert Member
- Aug 29, 2007
- 841
- 175
Ninasikitika sana kusema haya nitakayoandika hapa ndani lakini ndiyo hali halisi na inanikera sana na sina budi ku-share nanyi.
Hivi kweli hadi hivi sasa bado Tanesco ina sifa za kuitwa kampuni/taasisi ya umma pamoja na ubabaishaji wa miaka nenda miaka rudi!Kwa dhamana waliopewa na watanzania hadi hivi sasa hawajapata ufumbuzi wa nini tatizo linalosababisha umeme uwepo kwa mgao?!Binafsi,naamini tatizo/matatizo wanayajua ila ni kwamba hawataki kufanya kazi ni hii ni kutokana na kutokuwepo kwa mshindani katika sekta ya uzalishaji umeme.
Yaani haiingi akilini kwa miaka yote hiyo umeme unakuwa ni kitu cha msimu wakati sayansi haiamini suala kama hilo kuwepo kwa msimu katika matumizi ukizingatia tuko katika kizazi cha sayansi na teknolojia;mbaya zaidi wamesaini mikataba na makampuni matano:Songas.aggreko,IPTL,Dowans,Richmond yote haya ili kuongeza nguvu katika uzalishaji umeme na huku ya kitu mamilioni ya Tshs kwa kazi hiyo halafu bila aibu wanasimama mbele ya vyombo vya habari wanatutangazia mgao wa umeme!!
Kuliko kupoteza fedha katika haya makampuni si bora wangewekeza katika uzalishaji wa umeme kutoka baharini;wakapate somo India kuhusu hilo.Sijawahi kusikia kina cha bahari kimepungua kama wanavyozungumzia vyanzo vyeo vinavyoandamwa na matope.
Hivi kweli,wanafanya kazi ama wanauza sura kwenye magari na majengo ya kampuni yetu ambayo wameifanya ionekane nuksi kwa watanzania na wageni wanaofikiria ni kwa jinsi gani katika hali kama hiyo waje kuwekeza nchini Tanzania huku miji/majiji yakiwa giza na kuandamwa na uchafuzi wa mazingira kwa moshi na kelele za majenerata;sijui wanategemea maisha yetu yawe vipi kiafya na kiuchumi?
Siku zote hali ya hewa ya nchi yetu wanaijua;halafu bado wanaendelea kutegemea umeme wa nguvu za maji.Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani walivyokuwa hawako serious na kazi zao ndani ya kampuni.
Nimesikitishwa sana kwa jinsi kampuni inavyoona fahari kujitokeza mbele ya vyombo vya habari na kuutangazia umma wa watanzania ratiba ya mgao wa umeme;halafu mgao wenyewe unaendeshwa kiupendeleo.Na mfano hai,ni eneo fulani ukishuka Sinza kumekucha tangu mgao uanze hilo eneo halijawahi kukumbwa na dhahama hiyo wakati maeneo yaliyojirani na huo mtaa kila siku umeme unakatwa halafu mbaya zaidi ni usiku tu.
Na niamaini tangu uhuru hadi hivi sasa hawana kitu cha kujivunia kimaendeleo katika nchi hii tangu wapewe majukumu ya kuwa kampuni pekee inayozalisha umeme hapa nchini Tanzania.
Ni kawaida kwa mtu mwenye akili zake timamu kuweza kuchagua na kukikubali kitu kizuri na kukataa kibaya.Binafsi,siwakubali hata kidogo katika utendaji wa kazi zao hadi hivi sasa.