Glue
Senior Member
- Jan 14, 2011
- 156
- 49
Jamani wana JF wenzangu,
Naomba tuungane kupaza sauti zetu ili serikali ione sababu ya kufuatilia tatizo la TANESCO kwa wana Lindi.
Mimi binafsi si mkaazi wa Mkoa wa Lindi ila nimekuwa nikisafiri mara kwa mara kuja katika mkoa huu. Toka nianze kuja Lindi sijawahi kuona hata siku moja ambayo umeme haujawahi kukatika.
Na sio kukatika kwa akili, umeme unakatika kila baada ya dakika kadhaa. Kama ni tatizo la kiufundi basi ungekuwa unakatika kwa muda maalum na sio kukatika katika huku kusiko kuwa na formula.
Tafadhalini TANESCO muangalie hili tatizo kwani linarudisha nyuma maendeleo ya wana Lindi kwa kiasi kikubwa na pia ni kero sana kwa wananchi hususani katika kipindi hiki cha joto.