TANESCO mkoani Pwani yawanasa wezi 7 kwa tuhuma za kujiunganishia umeme kinyemela

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Shirika la ugavi wa umeme Tanesco Mkoani Pwani limewakamata watu saba kwa tuhuma za wizi wa umeme katika eneo la kwamfipa Wilayani Kibaha ambao walikuwa wamehujumu miundombinu kwa kujiunganishia umeme kinyemela kinyume cha utaratibu.

Akizungumzia kuhusina na tukio hilo Afisa Usalama wa Tanesco Mkoa wa Pwani Herny Byarugaba amesema kwamba kubainika kwa watu hao waliokuwa wanaiba umeme kumetokana baada ya kupatiwa taarifa kutoka kwa wananchi wasamalia wema wa eneo hilo.

Byarugaba amesema kwamba wezi hao walikuwa wamezichimbia nyaya za umeme chini ya barabara ya kuusambaza katika baadhi ya maeneo ikiwemo maduka, mabanda ya kuonenyeshea video hali ambao amedai ni hatari kwa usalama wa maisha ya watu kwani kunaweza kutokea majanga ya kuungua kwa nyuma za watu na kupoteza maisha yao.

“Sisi tumepata taarifa hizi kutoka kwa wananchi wasamalia wema kwa hiyo sisi kama tanesco tukaamua kufanya msako mkali katika eneo hili la kwa mfipa na kuweza kukuta wateja wetu wameamua kutumia njia za kinyemela kwa kuiba umeme na mbaya zaidi nyaya wamezipitishia chini kabisa ya barabara hivyo hali hii ni hatari sana watu wanaweza kupoteza maisha,”alisem Byarugaba.

Aidha alibainisha kwamba kutokana na kujiunganishia umeme kinyume na taratibu kunaweza kuleta madhara makubwa kwa wananchi kwani pindi mvua inaponyesha na nyaya hizo zikiwa zimechunika maji yanashika umeme na hivyo kunaweza kusababisha hatari kubwa sana.

Pia Byarugaba aliongeza kuwa Shirika la Tanesco limekuwa linapata hasara kubwa na kupoteza mapato yake kutokana na baadhi ya watu kuamua kufanya vitendo vya hatari vya kuhujumu miundombinu yao pamoja na kuiba umeme.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya mtaa kwamfipa Juma Tanga ambaye alifika eneo la tukio alisema kwamba amesikitishwa sana kuona baadhi ya wananchi wake kushiriki kuiba umeme kinyume na taratibu na kuwataka waachane na vitendo hivyo kwani ni hatari kwa usalama wa maisha yao.

Mwenyekiti huyo alisema kwamba katika kukabiliana na hali hiyo atahakikisha anaweka mikakati ya kuwaelimisha wananchi wake katika mikutano mbali mbali kuhusina na madhara ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na kujiunganishai umeme bila ya kuzingatia taratibu zilizowekwa na wahusika wenyewe.

Naye Meneje wa Tanesco Mkoa wa Pwani Martin Madulu ametoa tahadhari kwa wananchi wote wa Mkoa wa Pwani kuachana kabisa na tabia ya kujiunganishia umeme pasipo kuwatumia wafanyakazi husika wa tanesco na badala wake wahakikishe wazingatie taratibu katika kuunganishiwa umeme katika sehemu za biashara pamoja na nyuma za kuishi.

Aidha katika hatua nyingine Mejeja huyo aliwataka wananchi kujihadhari ya matapeli ambao wanajifanya ni wafanyakazi wa shirika hilo na endapo wakiwabaini watoe taarifa mapema katika vyombo vinavyohusika ili sheria iweze kufuata mkondo wake.
 
Watu huwa wanaamua kufanya hivi kutokana na utaratibu mbovu uliopo kwa baadhi ya ofisi za Tanesco ,utakuta mtu anatatizo la umeme anatoa taarifa Tanesco ,zaidi ya siku 3 wataalamu bado hawajaja kumhudumia,pia gharama za kuunganishiwa umeme inapaswa zishushwe ili watu waweze kufurahia Huduma za Shirika lao tofauti na ilivyo sasa gharama za kuunganishiwa umeme ni kubwa sana pia bado ukifanikisha kuunganishiwa gharama za uendeshaji nazo bado ni kubwa mfano service charge.Ombi langu kwa serikali ijitahidi kupunguza hizi gharama ili watu wengi waweze kupata Huduma kwa gharama Nafuu.
 
Watu huwa wanaamua kufanya hivi kutokana na utaratibu mbovu uliopo kwa baadhi ya ofisi za Tanesco ,utakuta mtu anatatizo la umeme anatoa taarifa Tanesco ,zaidi ya siku 3 wataalamu bado hawajaja kumhudumia,pia gharama za kuunganishiwa umeme inapaswa zishushwe ili watu waweze kufurahia Huduma za Shirika lao tofauti na ilivyo sasa gharama za kuunganishiwa umeme ni kubwa sana pia bado ukifanikisha kuunganishiwa gharama za uendeshaji nazo bado ni kubwa mfano service charge.Ombi langu kwa serikali ijitahidi kupunguza hizi gharama ili watu wengi waweze kupata Huduma kwa gharama Nafuu.
Rea imekufa subiri uone kama gharama zitapungua au kuongezeka.
 
Tanesco ni kuligawa tu wao wazalishe na kusafirisha, inshu ya kusambazia wateja wapewe makampuni binafsi hii italeta customer care safi sana
 
Sio wezi bali wamecheleshewa huduma maana hawa tanesco nao hujiona Kama miungu watu kwa sababu hawana kampuni shindani
 
Back
Top Bottom