TANESCO Misungwi/Nyamagana mnakera

G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
6,565
8,427
Mimi ni mkaazi wa Usagara wilaya ya Misungwi jijini Mwanza.naomba tu kukulizeni Tanesco..hivi mnafanya nini muda ambao ndiyo giza limeingia tunahitaji mwanga ninyi mnakata umeme?jana niliona tangazo linapita huko Whatsapp kua mtakata umeme leo 26/3/2019 kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni.lakini umeme umekuwepo mchana kutwa na kufika saa moja tu jioni umeme mmekata mpaka hivi naandika hapa ni 23:34pm tupo kwenye kwenye giza jamani.nalazimika kusema haya maana hii ni tabia iliyozoeleka,hivi kwa nini kwanza umeme ukatike?nini hamuwezi kurekebisha miaka yote hii?

1. Kuna siku nimetoaa taarifa za tatizo nyumbani kwangu na nilipokelewaa vizuri tu na mtoa huduma kwa namba ya Tanesco Nyamagana pale Mkolani na nikaambiwa mafundi watakuja lakini walikuja usiku na mbaya zaidi nilipokua naongea na huyo mti ambaye bahati mbaya sikuweka kumbukumbu ya jina lake,alikua ananijibu vibaya kwenye simu ninapomuelekeza,mala anikatie simu na kuonyesha ni kama hiyo kazi analazimishwa.nilihudumiwa kwa kero na machukizo,kitu hiki hiki kilimtokea jamaa yangu anaeishi Kisesa na nikachukulia hii ndiyo tabia yenu.ni kero,fanyeni kwa moyo kama mlivyoihitaji kazi

2. Kulitokea tatizo siku chache zilizopita pia,kiupepo kidogo tu nguzo zikalala na hawakuonekana kushughulikia tatizo siku tatu mfululizo hatukua na umeme hata kidogo.

Kwa machache haya ktk mengi hebu jirekebisheni aisew,sisi ni wateja na hamtupi umeme bure.acheni kuuangusha uongozi wa sasa wenye bidii na maarifa ya kuhakikisha taifa letu linakwenda sawa,ila ningekua nina uwezo mimi kama mimi ningeingiza mashirika hata kumi ya kuuza umeme hapa nchini,ninyi Tanesco mmetuchosha zaidi ya kutuchosha.

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Back
Top Bottom