Maeneo ya Mbagala yote naona tukae kimya,
Mbagala kumekuwa na tatizo sugu la kukatika kwa umeme kila siku jioni na kurudi mtu unapokuwa umeshalala usiku kwa muda mrefu, lakini cha ajabu, wakati wa kampeni ulipoanza, umeme haukuwa unakatika, hadi tukaanza kuwashukuru tanesco kwa kurekebisha tatizo la kukatika katika kwa umeme.
Cha ajabu ni kwamba, toka raisi aapishwe, tumerudi tena kwenye mgao usio na mpangilio kila siku jioni, mbaya zaidi unakatika almost usiku mzima na kusababisha hasara kuwa sana kwa sisi watumiaji. Ukiwapigia simu tanesco kuwauliza au hata ukienda ofisini kwao (kitu ambacho nimefanya) na nimeandika barua kuonyesha kulalamika kwangu kwa kukatikakatika kwa umeme huku, jibu wanalonipa ni simple,, Kuna tatizo katika njia za umeme, mafundi wanafanyia kazi, utarudi.
Swali la msingi, je? tatizo hili katika njia linachagua wakati wa kampeni na wakati usio wa kampnei? na je? kwa nini mchana haukatiki (muda ambao binafsi sipo nyumbani) na unakatika usiku (muda ambao nipo nyumbani nataka nitumie umeme?
Nimekasirika hadi sasa nimeamua hata kwa mkopo, nitafute suluhisho langu kwa suala hili la umeme, siwezi kuendelea kuishi wanavyotaka tanesco, no way.