Verily Verily
Senior Member
- Jan 4, 2007
- 188
- 143
Heshima kwenu wakuu,
Hii thread iwe Maalum kwa Maoni, Ushauri na Mapendekezo mbalimbali au kutoa Taarifa na changamoto Mbalimbali kwa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO
Vilevile unaweza kutembelea thread hii =>Namba za simu za mameneja wa Wilaya (116) wa TANESCO kwa kila Mkoa
Kwa upande wangu Mimi namuomba, Mkurugenzi mpya wa TANESCO ajipange kudhibiti wizi wa umeme nchi nzima.
1. Mkurugenzi mpya Ndugu Tito Mwinuka ana jukumu kubwa mbele yake.
2. Upatikanaji wa Umeme wa uhakika na wa kutosha ndio ufunguo wa Tanzania ya viwanda.
3. Zaidi ya 50% ya watumiaji wa umeme nchini wamejiunganishia umeme kiholela na hivyo kusababisha hasara kubwa kwa shirika. Kwa hali ilivyo shirika haliwezi kufanya maendeleo iwapo wizi huu utaendelea.
4. Kuna mitaa ya pembezoni mwa jiji na mikoa kwa mfano utakuta karibu nyumba zote zinatumia umeme wa wizi.
5. Mkurugenzi mpya, akijua ana jukumu la kuipeleka nchi kwenye uchumi wa viwanda ajipambanue, ajitofautishe na watangulizi wake. Aanzishe mpango endelevu wa kutembelea nyumba kwa nyumba mtaa kwa mtaa akianzia miji mikubwa mpaka vijini na kuwachukulia hatua kali wezi wa umeme. Atoe adhabu ambayo watu hawatatamani kuiba umeme kamwe. Mpango huu uhusishe vyombo vya dola na sheria. Ikiwezekana bunge litunge sheria mahsusi ya kuliokoa taifa na wizi wa nishati ya umeme.
6. Sanjari na kukamata wezi nchi nzima atathimini bei za umeme ili wananchi hata wa kipato cha chini waweze kulipia badala ya kuiba.
7. Tafadhali Mkurugenzi ndugu Tito Mwinuka na TANESCO jibu hoja hizi kwa faida ya nchi.

Ninaweza kumsaidia kumuonyesha nyumba 3 Dar es salaam zinazotumia mita moja ya umeme na kwa mwezi hutumia umeme usiozidi shilingi 4000.
Pia Mwanza kuna mtu kaunganishiwa umeme bila mita na yeye kafungua tanesco yake kasambaza umeme ktk nyumba kibao,mwisho wa mwezi hao wateja humlipa yeye kiasi cha 10000 kila mmoja bila kujali matumizi yao maana hakuna mita,na yeye muhusika mkuu hutoa posho kwa baadhi ya watumishi wa tanesco wasio waadilifu
Hii huduma ina mambo mengi sana, vifaa ghali sana. wateje wezi wezi sana (wajanja wajanja), kufanikisha ulinzi na usalama wa huduma inaweza kukugharimu sana na kushindwa kufikia hata wanayofikia kwa sasa.
nadhani, elimu itolewe ya kutosha kwa wananchi, waeleweshwe umuhimu wa kulipa na kuacha wizi wa nishati hii muhimu kwa maisha yetu. kila mtu awe mhimili wa ulinzi na usalama wa miundombinu ya umeme.
Pia wangerekebisha tariff zao za manunuzi ya umeme toka kwa wazalishaji binafsi, wanunue kwa bei nzuri ili watu wengi wazalishe na kuwauzia TANESCO.
Nakumbuka hili (Mbeba nguzo mwizi, msoma meter mwizi, karani mwizi, mkurugenzi mwizi, hata mlipa bill (beneficiary)naye mwizi unadhan hapo kuna shirika????????)
Wanabodi kutokana na niliyoyashuhudia tanesco ya kigamboni,ni wazi kabisa jipu ambalo linahitaji kutumbuliwa.
Watu wengi wanaohitaji kufanyiwa survey ili wapate huduma hiyo,mteja huchangishwa kiasi kisichozidi shilingi za kitanzania 7,000/= ili kukodi gari litakalowawezesha kupita maeneo yao kupatiwa huduma hiyo.
Mtu yeyote asiekuwa na kiasi hicho ataishia kupigwa kalenda mpaka ajute kuisikia tanesco.
Serikali yetu tukufu wakati inafanya juhudi ya kuongeza pato la taifa, kwa kuhimiza mashirika ya uma kutafuta vyanzo vipya vya mapato tanesco kigamboni wanazirudisha nyuma jitihada hizo.
Kuna lundo la wateja ambao pamoja kuwa na pesa yao mkononi kwa ajili ya kupatiwa huduma lakini bado wananyanyasika na kutothaminiwa.
Nitowe wito kwa wizara husika wajaribu kufuatilia mwenendo wa tanesco kigamboni dhidi ya wateja wao katika kutoa huduma kwani ni jibu. Nina ushahidi wa kutosha juu ya hili ikiwemo audio na video.
Nitakribani mwaka mpango wa kuweka umeme kweye baadhi ya maeneo umekuwa ukitekelezwa kwa kusua sua.
Tumeshuudia nguzo kubwa wa umeme mkubwa (HT) zikichukua takribani miezi nane na zaidi. Usambazaji wa nguzo za umeme mdogo zimechukua miezi karibia mitano. Transforma zilichelewa mpaka watu wakatishia kuandamana ndo tukaona zina tundikwa.
Sasa cha kushangaza pamoja na juhudi zote hizo upatikaji wa META umekuwa mgumu sana. Vishoka wa Tanesco wanaitaji mpaka shilingi laki moja na nusu ili upata hiyo meta. Ili hali umeme watu wemeisha lipia shilingi laki tatu na elfu ishirini na tisa.
Tafadhali mkuu njoo hapa Tanesco Mbeze uwatumbue hawa watendaji. Tumechoka na majibu yao yanayokatisha tamaa.