Tanesco Kimara huduma ni mbovu

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,409
13,260
Nimefika Tanesco ofisi za Kimara juzi na jana nikashindwa kupata huduma kutokana na kukatika kwa umeme kufuatia matengenezo ya laini kubwa yanayofanywa na shirika. Jambo la kushangaza ofisi kubwa kama ile haina jenereta la dharura ili kuwahudumia wateja umeme anapokatika. Ofisi ili inahudumia mamia ya watu ambao walilazimika kurudi nyumbani na pesa walizokusudia kufanya malipo mbali mbali ya huduma za umeme ikiwemo kulipia maombi mapya kama ilivyokuwa kwangui na kununua Luku.

Wateja wengi tuliokuwa pale tulishanga ni kwa vipi Tanesco ikubali kulipa watu wasiofanya kazi za kawaida za ofisini kwa kisingizio cha kukatika kwa umeme. HIvi jenereta la kuondesha kompyuta za ofisini tu lina gharimu shilingi ngapi hadi washindwa kununua? Wateja tuliokuwa na hasira ya kupotezewa muda tulimuuliza meneja kuhusu ofisi yake kubwa kama ile kukosa jeneraeta wakati hapo jirani mita chache kutoka ilipo ofisi yake kuna kinyozi kawasha jenereta ana mnyoa mteja ambao anamlipa sio zaidi ya 2000 wakati sisi tuna lazimika kurudi nyumbani na malaki ya hela tulizokusudia kulipa tanesco lakini tumekwama sababu ya kukiosa umeme katika ofisi za shirika la umeme? Hakuwa na jibu zaidi ya kujiuma uma tu yule mzee wa watu.
 
Back
Top Bottom