Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Nimesikia kwa kuambiwa kuwa magari yote ya TANESCO ya mikoa ya Pwani na Dar es Salaam (hasa yale ya Emergency) yanajaza mafuta yake katika kituo kimoja cha mafuta. Kituo husika cha kujaza mafuta hayo ni cha TOTAL cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kona ya kwenda na kutoka Mwenge).
Ndiyo kusema, magari yote ya TANESCO ya Wilaya zote za Dar es Salaam na Pwani yanajaza mafuta yake pale. Kuyaleta magari ya Chalinze, Bagamoyo na Kisarawe kuja kujaza mafuta pale ni ubadhirifu wa fedha. Kwa umbali wake, magari hayo hutumia mafuta mengi wakati wa kuja na kuondoka kujaza mafuta.
Nawauliza TANESCO ,jambo hili lina ukweli wowote? Kama ni kweli, fanyeni hima kurekebisha jambo hili. Kumbukeni kuwa pesa zinazotumika TANESCO ni pesa za umma.Hata kama ni makubaliano, makubaliano yanaweza kufanywa na vituo vya mafuta vya maeneo ya karibu ya Wilaya husika.