naomba nisahishishwe kama kumbukumbu zangu hazipo sahihi.
Tarehe 15/02/2012 Tanesco walipandisha rasmi bei ya umeme kwa 40% baada ya kukubaliwa na EWALA. hiyo parcentage iliyoongezeka ni kwa ajili gani?
Mwaka jana bajeti ya wizara ya nishati na madini ilipokataliwa kupitishwa na bunge iliposomwa kwa mara ya kwanza ,walienda na kuirekebisha na kuweka hela nyingi sana kwenye tanesco ndipo wabunge vilaza wetu walipoipitisha kwa kelele, au zile namba walizoongeza kwenye bajeti ni za uongo?
Je? Suluhisho ni mgao? ikishondikana tunakoenda ili kutupunguzia kulaumu, wauze unit moja ya umeme hata kwa Tshs. 5,000 ili wenye pesa waendelee na maisha na asiye nayo awe anatumia umeme kwa ajili ya taa tu ili tujue moja nchi haina umeme.
Na hizi dharura watanzania tulishazikataa, sijui kwa nini wanaendelea kulala nazo tu nakuzaa nazo hadi zinatuzidishia matatizo namna hii
Nimechoka kulaumu uzembe wa watu wengine jamani, hivi hakuna mtu kweli wa kutimiza wajibu wake?