Wanabodi,
Inasemekana kuwa Shirika la Ugavi wa Umeme nchini Tanesco limeshindwa kununua mafuta kwa ajili ya mitambo ya kuzalisha umeme wa dharula.
Kwa mujibu wa mikataba ya uzalishaji wa umeme wa dharula ambayo shirika hilo limeingia na makampuni kadhaa ya kuzalisha umeme wa dharula ni kuwa Tanesco inawajibika pamoja na kulipia gharama za matengenezo, pia itatakiwa kununua mafuta ya kuendeshea mitambo ya kuzalisha umeme kwa makampuni hayo.
Makampuni hayo ni pamoja na Symbion, Aggreko na IPTL.
Kutokana na ukata huo, hadi sasa mitambo ya makampuni kadhaa ya kuzalisha umeme wa dharula imesimamisha shughuli za uzalishaji wa umeme huo wa dharula.
Mitambo ambayo imesimamishwa hadi sasa ni Symbion Dodoma (50MW), Aggreko Dar (50MW) na IPTL Dar (100MW).
Kutokana na mitambo hiyo kusimamisha uzalishaji, tayari maeneo kadhaa yameshaanza kuonja machungu ya mgawo wa umeme. Mgawo huu unatarajiwa kuwa mkali zaidi kwa kadri siku zinavyozidi kwenda kwani hata hali ya kina cha maji kwenye mabwawa ya kuzalishia umeme ya Mtera na Kidatu si nzuri sana.
Pamoja na kuwa Tanesco inakaribia kukamilisha ujenzi wa mtambo mwingine wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia pale Ubungo-Dar (100MW), lakini mtambo huo huenda usiweze kuzalisha umeme kwani inasemekana kuwa gesi iliyopo haitoshi kuweza kuongeza mtambo mwingine labda kama baadhi ya mitambo ya Symbion ambayo sasa inatumia gesi itaanza kutumia jet fuel. Tatizo linarudi tena palepale, mafuta hayo ni gharama kubwa sana na Tanesco inaonekana kushindwa kumudu gharama za ununuzi wa mafuta hayo.
Miradi mingi ya ujenzi wa vituo vya kuzalisha umeme ilikuwa inategemea ule mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Ubungo Dar es Salaam. Lakini inaonekana kuwa mradi huo wa gesi tayari umeshaingia mushkeli. Mipango ilkikuwa bomba hilo liwe limekamilika ifikapo Desemba 2012. Hadi sasa hakuna kazi yoyote iliyoanza katika utekelezaji wa mradi huo.
My take:
Huu ni mwiba mwingine kwa watanzania.