TANESCO hii ni staili gani ya biashara jamani?

Translator

JF-Expert Member
May 19, 2017
286
297
Hivi TANESCO wana tofauti gani na mamantilie anayeuza chakula na ana duka la mafusuria?

Ukienda kusema, “Nipe wali samaki,”
Anakwambia, “Nunua sufuria nikupikie”

Unanunua, anapika, anakutengea.
Kisha anasema, “Sahani shilingi 3000.”

Unakula na kulipa tena.
Ukimaliza kula unamwambia, “Nimemaliza nipe sufuria yangu.”

Anakutazama kwa dharau kisha anasema, “Sufuria yako! Umelogwa nini?”

Inaonekana kuna mgando wa hatari wa mawazo kwenye nchi hii.

Hivi watu wooooooote TANESCO hakuna aliye creative hata mmoja?
Je, nchi hii creativity ni katika kubuni njia za kupatiana posho tu?
Na pamoja na kuwa soko loooooote nchini ni lenu lakini bado mnathubutu kulia ukata!

Shame on us!

upload_2017-7-26_12-19-17.png

 
Huwa nashangazwa sana na system hii.Yan service yao ila unanunua kila kitu.Kuanzia waya wao ule,bracket,nguzo,unalipa service chaji sijui na mengine mengi.Yan wanaboa sana hawa jamaa ni sera mbovu sana yan.
LAZIMA WAWE NA MSHINDANI KIBIASHARA HAWA MBURURA
 
Kweli kabisa Perfectz . Upinzani ndio komesha ya uzembe na kiburi chote; kama walivyonyooka simu na posta.
 
Swali je vile vitu ulivyo lipia kama nguzo, mita n.k vikiharibika huwa wanakuja kukutoza hela tena? Kama hapana unadhani hua wanavitoa wapi pindi wanapokuja kubadilisha vilivyo haribika? na kwa fedha ya nani?
 
Wizi mtupu ....
Hakuna shirika la umma lililo safi ..kote kunanuka ubadirifu ..
Ila tuwe wapole mjomba amesema anataka kunyoosha nchi
 
Swali je vile vitu ulivyo lipia kama nguzo, mita n.k vikiharibika huwa wanakuja kukutoza hela tena? Kama hapana unadhani hua wanavitoa wapi pindi wanapokuja kubadilisha vilivyo haribika? na kwa fedha ya nani?
Yaani soko la nchi nzima ni lako 100% ushindwe kupata faida? Hiyo si halali kabisa. Kwanza kwa soko hilo, mimi naamini wangeweza kuwa wanatanguliza kabisa nguzo hata kwenye makazi mapya ili kuvuta watu kuhamia na kujenga nyumba zao, hivyo kupanua wigo wa mapato yao.
 
Back
Top Bottom