DOKEZO TANAPA wekeni wazi taarifa za ubadhirifu wa Fedha za Umma ili kama ni kweli wahusika wawajibishwe

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hali si shwari ndani ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), baada ya kubainika kuwepo matumizi mabaya ya mabilioni ya fedha za shirika, balaa hilo limegundulika baada ya timu mbili za Wakaguzi wa Hesabu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya ukaguzi kwa maelekezo ya Waziri wa Wizara hiyo kubaini "madudu".

Inaelezwa kuwa sehemu kubwa ya fedha hizo zinatajwa kuchepushwa kupitia Kampuni tanzu ya TANAPA.

Kuna taarifa za matumizi mabaya ya fedha, ambapo timu ya kwanza ya wakaguzi kutoka Wizara ya Utalii ilibaini kiasi cha Shilingi Bilioni 14 lakini taarifa za uhakika zinasema Wizara ilituma timu ya pili wiki chache zilizopita, ambapo timu hiyo inatajwa kubaini Shilingi Bilioni 19.

Taarifa zinasema sehemu kubwa ya fedha hizo za umma, zilienda kampuni tanzu, kampuni ambayo Mtendaji Mkuu (CEO) akalazimishwa kukabidhi ofisi siku chache zilizopita, pamoja na taarifa kuwa kulikuwa na mkakati wa kumuongezea muda.

Pia, ubadhirifu huo umefanywa chini ya uratibu wa aliyekuwa bosi kubwa wa TANAPA, ambaye naye amelazimishwa kustaafu ghafla baada ya ukaguzi huo wa Wizara.

Alipaswa kustaafu tangu Mwaka 2025 lakini aliendelea kuwa ofisini kwa nguvu ya baadhi ya vigogo Wizarani ambao nao wanatajwa kuwa wanufaika wa mnyororo wa fedha za ubadhirifu kutoka TANAPA.

Hata hivyo, kulazimishwa kustaafu ghafla kwa vigogo hao wawili wa TANAPA, kumeleta mshtuko kwa baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo, hususan wa Kurugenzi ya Fedha, mpaka sasa inadaiwa Maafisa wawili kitengo cha fedha wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi.
 
Tanapa na Kinapa sasa inamilikiwa na Kizmkazi.
Wizi mtupu!
 
Serikali ya ss imejaa mijizi mno. Na mbaya zaidi yakiiba Yana tesa tu mjini kiongozi. Mkuu anasema tuwaseme mpk waone aibu!!
Kazi ni kipimo cha utu
 
TANAPA ni kitovu cha rushwa, ubadhirifu na ulaji wa fedha toka wakati wa Mwakilema aliyeondolewa kwa madudu na kuwa Mkuu wa Wilaya huko Tanga.
 
Tanapa ni sehemu ya upigaji mkubwa huko wakitaka ukaguzi wa wazi wampeleke CAG hapo hizo wanazosema ni ndogo wanachagua watu wa kuwakagua wakati CAG yupo ni kazi yake atoe na taarifa mbona mtakimbia hapo...
Kama tumeweza azima majaji napendekeza tuazime CAG wa Rwanda ama Ghana wakatusaidie
 
TANAPA ni kitovu cha rushwa, ubadhirifu na ulaji wa fedha toka wakati wa Mwakilema aliyeondolewa kwa madudu na kuwa Mkuu wa Wilaya huko Tanga.
Rushwa, ubadhirifu, ufujaji, utapeli TANAPA ni toka kitambo... Kabla hata ya Mwakilema. Sema yule mwamba alichongewa kwa Mkaza mwanae Samia wakigombania gari la kifahari msaada kutoka FZS.
 
Serikali ya ss imejaa mijizi mno. Na mbaya zaidi yakiiba Yana tesa tu mjini kiongozi. Mkuu anasema tuwaseme mpk waone aibu!!
Kazi ni kipimo cha utu
Mkuu;
Wazanzibari wameteuliwa maeneo nyeti kimkakati.
Wanakwapua WaTanganyika wakiwa usingizini
 
Rushwa, ubadhirifu, ufujaji, utapeli TANAPA ni toka kitambo... Kabla hata ya Mwakilema. Sema yule mwamba alichongewa kwa Mkaza mwanae Samia wakigombania gari la kifahari msaada kutoka FZS.
Rushwa TANAPA ni jadi, hata miradi ya World Bank.
Mradi wa uwanja wa ndege Mikumi nasikia mzawa aliyeshinda kazi akatupwa kapuni na akapewa "mchina wao" wa kula naye, ambaye kaboronga kazi kaboronga kazi
 
Ni hatari...
Kwa sasa SSH kaamua kujilimbikizia kila fursa...
Anapora sites kwa kwenda mbele!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…