TAMWA ZNZ: Madawati ya kijimsia kwenye vyombo vya Habari ni muhimu kulinda Haki za wanawake

G-Mdadisi

Senior Member
Feb 15, 2018
157
99
Chama cha Waandishi wahabari Waanawake Tanzania (TAMWA-ZNZ) kinaviomba vyombo vya habari Nchini kuweka madawati ya kijinsia ili kushughulikia kwa ukaribu masuala hayo na hivyo kuimarisha haki za zawanawake na watoto.

TAMWA-ZNZ hivi karibuni ilitembelea vyombo vya habari 14 (10 kutoka Unguja na 4 kutoka Pemba) vikiwemo vyombo vya Habari vya uma, binafsi na radio za kijami.

Afisa wa ufuatiliaji na Tathmini wa TAMWA- ZNZ Bwana Mohammed Khatibu alisema katika ziara hiyo iliyoanza tarehe 24 Mei hadi 21 Juni , TAMWA,ZNZ ilikuta vyombo vya habari vitatu ambavyo vimeweka madawati ya kijinsia na vilivyobaki bado havikuanza utaratibu huo.

Alisema pia baadhi ya vyombo vya habari asilimia 33% vilikuwa na sera ya jinsia ambayo ni muhimu kwa usawa wa kijinsia lakini nyingi zao zilikosa mipango kazi wa utekelezaji wa sera hiyo.

Hivyo, alisema TAMWA- ZNZ itakaa pamoja na vyombo hivyo kuandaa mpango kazi wa utekelezaji pamoja na kuweka na mfumo maalum wa kuripoti matokeao yake.

Vyombo vya habari vikiwa na mifumo ya kijinsia vitasaidia sana kutoa habari ambazo zinauwiano sawa wa kijinsia, kutafuta mambo ambayo yanaawaathiri wanawake pamoja na kutoa sauti za wanawake na watoto wa kike hivyo kuongeza kujiamini kwao; jambo ambalo ni muhimu katika safari yao ya uongozi.

Uchambuzi wa kihabari uliofanywa na TAMWA- ZNZ mwaka jana (2021) ulioonyesha kuwa ni asilimia 25 tu ya habari ndiyo imebeba sauti za wanasiasa wanawake na hivyo kuna haja ya kuleta uwiano hasa kwa vile wanawake ni zaidi ya asilimia 50 ya wakaazi wa Zanzibar kwa mujibu wa takwimu za sensa ya mwaka 2012 na makadirio yake.

Tanzania pamoja na Zanzibar zimeridhia Itifaki mbali mbali za kimataifa pamoja na za kikanda ili kuhalikisha inatekeleza azimio la kufikia usawa wa kijinsia ikiwemo uwakilishi wao katika vyombo vya maamuzi na sauti zao katika vyombo vya habari.

Hata hivyo, TAMWA- ZNZ inashukuru kwa mapokezi iliyopewa na vyombo vya habari mbali mbali, ambapo pia vimekubaliana kuweka madawati na sera za kijinsia pamoja na kuweka mikakati ya utekelezaji wake.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Zanzibar, Bwana Salum Ramadhan Abdalla ameeleza utayari wa Shirika lake katika kuimarisha habari za kijinsia ikiwemo kuweka mfumo wa kumbukumbu na ufuatiliaji wa masuala ya kijinsia.

“Tupo katika mchakato wa kutengeneza sera ya jinsia, hivyo haya yote tutayazingatia ili tuweze kuripoti habari za wanawake kama wasemaji, lakini pia kama walengwa wa taarifa zetu”, alisema.

Chama cha waandishi wahabari waanawake Tanzania (TAMWA-ZNZ) kinaishirikana na Jumuiya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumiya ya Utetezi wa Jinsia na Mazingira Pemba (PEGAO) kupitia udhamini wa Ubalozi wa Norway nchini, kinatekeleza kwa pamoja mradi wa kuwainua wanawake katika uongozi na haki zao za kidemokrasia.
 
Back
Top Bottom