Tamko la chadema - mkoa wa singida, tupo tayari!

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO – CHADEMA MKOA WA SINGDA
TAMKO LA CHADEMA JUU YA UNYANYASWAJI WA HAKI YA KIDEMOKRASIA ANAYOFANYIWA MH.GODBLESS LEMA, KKIONGOZI WA UPINZANI NA MBUNGE WA HAI, MH. FREEMAN MBOWE, TUNDU LISSU (MBUNGE WA SINGIDA MASHARIKI), KATIBU MKUU DR. WILBROD SLAA, NA WANACHADEMA WENGINE ARUSHA NA TANZANIA KWA UJUMLA.


Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Singda, kimesikitishwa sana na utendajikazi wa Jeshi la Polisi, na hata mahakama za Tanzania usiozingatia sheria.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mkoa wa Singida kinasikitishwa sana na utendaji mbovu wa Jeshi la Polisi.

Tumesikitishwa na yaliyotokea Arusha na kweli jeshi la polisi haliwezi kuepuka lawama hizi. Arusha kulitokea mvutano kati ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufungua matawi.
Jeshi likawanyima kibali halali cha kufanya mkutano, eti wale vijana wa CCM wakaamua kutumia walinzi wa kampuni binafsi. Jeshi la Polisi halikuona? Kama liliona mbona halikuwachukulia hatua? Waliogopa mashati ya kijani, wakaamua kuificha ile kaulimbiu yao ya utii wa sheria bila shuruti. Ni ujinga.
Baadaye wanajidai kuanza kuwatafuta eti walisema maneno ya uchochezi mkutanoni. Kwanini hawakuwakamata hapo hapo? Hakuna makachero? Je, kila chama kikija na kampuni binafsi kulinda mikutano yake nchi itatawalika?
Polisi simamieni msimamo wenu kimaadili ya jeshi, si kiushemeji, kufahamiana, kihali ya kifedha na kivyama. Mnakokwenda mnatuharibia nchi”
Tujiulize haya, waliotoa taarifa kuwa Vijana wa Chama cha Mapinduzi wamefanya mkutano kinyume cha utaratibu ni polisi wenyewe. Tulijiuliza sana siku hiyo, iweje vijana wa Chama cha Mapinduzi watumie walinzi wa kampuni binafsi? Hivi itakuwaje kila Chama kikianza kuwa na walinzi wa kampuni binafsi?

Sikujibiwa. Tunauliza tena ilikuwaje vijana wa Chama cha mapinduzi wakafanya mkutano ndani ya mji bila kuwa na kibali? Polisi inakiri kuwa iliwanyima kibali cha kufanya mkutano lakini walifanya, wakalindwa na kampuni binafsi, wakamaliza wakaondoka. Tena wakatoa na Maneno ya uchochezi James Millya, Mwenyekiti wa Arusha, na Beno Malisa, kaimu Mwenyekiti wa UVCCM taifa wakatafutwa lakini hadi leo hawajafikishwa mahakamani. Kwa kosa hilo hilo la kukusanyika bila kuwa na kibali, Vijana wa Chama cha mapinduzi wapo nje, wanaendelea kutanua, hawana kesi mahakamani.

Lakini Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambaye yeye alifuatwa na wafuasi wake ili awajuze yaliyojiri Mahakani ana kesi Mahakamani, anapaswa kujibu. Tena mbaya zaidi, Vijana wa Chama cha Mapinduzi walifanya mkutano, ukahudhuriwa na watu. Mbunge Godbless Lema hakufanya Mkutano, aliondoka mahakamani kurudi ofisini, huku watu wakimdai awaeleze kilichojiri mahakamani baada ya Mahakama kushindwa kuweka vipaza sauti kama ilivyoahidi kabla ya siku ya kesi. Nani kati ya hawa ana kosa? Wale waliofanya mkutano bila kibali, au Yule aliyetoka mahakamani kurudi ofisini kwake na kusimama angalau awaambie ndugu zake kilichojiri mahakamani, baada ya mahakama kuwanyima ndugu zake haki ya kusikiliza kesi ya ndugu yao?
Wakati Godbless Lema anashtakiwa Mahakamani, sheria zilizopo ni zile zile kuhusu mikusanyiko ambazo ziliwaacha huru vijana wa CCM waliovunja sheria, watekelezaji ni wale wale askari wa jeshi la polisi wa Arusha, mahali ni pale pale zilipovunjwa sheria na vijana wa CCM , katika manispaa ya jiji la Arusha, Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ni Yule yule Zuberi Mwombeji, Mwezi ni huo huo ambapo vijana wa CCM wamefanya kosa zaidi wakaachiwa, lakini Lema akafikishwa mahakamani na sasa yupo rumande japo ni baada ya yeye kukataa dhamana. Wakati Lema anakamatwa kwa kosa hilo Nchi ni ile ile, Tanzania inayosema kuwa kuna demokrasia ya Vyama vingi, uhuru wa kujiunga na vyama vyovyote, au uhuru wa kuabudu. Wakati Lema anakamatwa na kufunguliwa mashtaka, Vijana wa CCM waliovunja sheria wakivinjari nje tunaambiwa katiba inayotumiwa na vyama vyote ni ile ile inayozungumzia usawa.
Kama hiyo haitoshi wamewadhalilisha viongozi wetu, kuwabambikia kesi kila mara. Tunashindwa kufanya shughuli za kisiasa kwa sababu ya jeshi la polisi. Imefikia hatua tunakata tama ya kufanya siasa za kidemorasia. Viongozi wetu wameenda Arusha baada ya jeshi lenyewe kuomba kuwa viongozi wetu wamwombe Lema atoke jela, alikubali ushauri wa viongozi wetu, lakini wamefika Arusha wamedhalilishwa na polisi tena. Je tutafanyaje shughuli za kisiasa katika Mazingira haya?
Lema aliambiwa dhamana ipo wazi je uamuzi huo ulibatilishwaje nje ya Mahakama mpaka tupangiwe muda wa kumdhamini ilihali dhamana ni haki ya mtuhumiwa?.

Jeshi la polisi limekuwa likifanya kazi kwa kutegemea maamuzi ya Viongozi wa CCM na ni bahati mbaya zaidi sisi hapa Singida muda sio mrefu tumeshuhudia Chama cha mapinduzi wakifanya mkutano nje ya muda, hawakuchukuliwa hatua zozote, lakini sisi tumekuwa tukikamatwa kila mara. Jeshi la Polisi Mkoa wa singida tuliwaandikia barua hawajajibu hadi sasa na kutomba radhi. Wataacha lini kufanya kazi wakipendelea Chama cha mapinduzi? Jeshi la polis indo linafanya nchi isitawalike. Tena kwa kutukandamiza sisi kufanya shughuli za kisiasa ni hatari zaidi.
Kwa kuwa matukio yaliyojitokeza Arusha 5/01/2011 na kusababisha watu watatu kuuawa yalitokana na Uzembe wa Jeshi la Polisi na Maelekezo ya Kipuuzi ya IGP Said Mwema, Na kwa kuwa tunaona maelekezo yote anayotoa IGP na Makamanda wa Polisi wengine Mikoani, ikiwamo Arusha na Singida ni mabovu yanayoonyesha kuwa anafanya kazi kwa maelekezo ya CCM, tunamtaka sasa IGP ajiuzulu, hafai kwa Usalama wa Raia na Mali zao anafanya kazi kwa misingi ya Vyama.Huyu sasa ni hatari kwa ustawi wa demokrasia na haki za binadamu. Pamoja naye ili jeshi la polisi nchini liheshimiwe tunaomba OCD wa Arusha aondolewe kazini haraka, na RPC wa Singida ajiuzulu. Hadi tunaandika tamko hili jeshi la polisi Mkoa wa Singida limeshindwa kutuandikia barua kujibu kwanini CCM walifanya Mkutano Singida nje ya Muda bila kukamatwa, tena katikati ya mji na kutoa matusi mazito kwa viongozi wakuu wa Chama chetu tena mbele ya Polisi . Kwa kuwa hii tulimwandikia kwa barua na anasuasua kujibu, na yanayotokea Arusha ni kama haya ya Singida. Kwa kifupi sisi tunasema tunapoteza imani na baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi. Jeshi ambalo limekuwa la ubadhirifu kila siku, lisilojishughulisha na maadili yake isipokuwa kunyanyasa watu, kuwasumbua viongozi wa CHADEMA. Viongozi wa CHADEMA tunapolalamika hatusikilizwi. Kiongozi wa CHADEMA Mkoani Singida alitishiwa kuuawa, lakini hadi sasa jeshi la polisi linasita kumchukulia hatua mtuhumiwa. Hali ilivyo sio njema sana, tunawaalika wananchi wa Tanzania kujilinda zaidi kwani jeshi limepoteza ladha yake kwa maadili linayopaswa kufuata. Baadhi ya Viongozi wa Polisi wamekuwa makada wa CCM waziwazi bila kificho, hii imeliharibu kabisa jeshi letu.

Watawala na Chama cha mapinduzi na serikali yake wawe makini sana katika kuwatumikia Watanzania kama walivyong`ang`ania kubaki madarakani kupitia uchaguzi mkuu uliopita pamoja na dallili zote zilizoonyesha kuwa walikuwa wamepoteza ushawishi kwa watanzania kwa kiasi kikubwa sana na wakijua wazi kwamba wakati wa kuwaburuza watanzania umekwishapita,Watanzania wa leo si wale wa miaka ya ndiyo mzee kwa kila jambo bila kuwa na uwezo wa kuhoji. TUTAUNGA MKONO HARAKATI ZOZOTE, WANANCHI WA SINGIDA NA WATANZANIA WAZALENDO TUUNGENI MKONO KUHOJI. HII NCHI NI YETU SOTE.

Josephat Isango-MWENYEKITI WA BAVICHA MKOA, NA KAIMU MWENYEKITICHADEMA MKOA WA SINGIDA
 
Naam..............
Utumwa noooooo..haki daimaaaaaaaa.Ccm jitafakarini,kuna siku kila mmoja atasimama kutoa hesabu ya mema na mabaya..nasema jitafakarini .bei ya dola leo ni 1745-1850...Uchumi wa TZ umekumbwa na nini???.wahusika hawaonii??,haya yote ni kutokana na kutoheshimu haki ya mtanzania..
 
karibuni kwenye mapambano ya kudai demokrasia ya kweli ya tanzania.
 
Ni tamko lililojaa ukweli ingawa kuna maneno makali kiasi na hii inaonesha ni jinsi gani watu walivyochoka na jeshi la Polisi kiasi kwamba hakuna mwenye imani tena na jeshi hili.
Hii ni nchi yetu sote na inatakiwa kila mmmoja wetu afuate sheria,si sheria itumike kwa mmoja huku kwa mwingine kuwe na visingizio kuwa usifanye mambo kwa kufuata mwenzio alifanya kama wewe,kauli kama hizi ndio huleta machafuko kwani zinaonekana kuegemea upande mmoja na hazina usawa.
Natambua baada ya tamko hili inawezekana kabisa huyu mwenyekiti akakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya uchochezi ila hata siku moja hawawezi kurudisha nyuma harakati za wapenda haki na maendeleo ya nchi hii ambao wanajitolea kila siku kuhakikisha nchi hii inatawaliwa kwa misingi ya usawa na kila mtu anapata haki sawa na hakuna matabaka.
 
Asante Iringa CDM kwa mshikamano na CDM Arusha.....we encourage mikoa mingine to follow suti..mpaka kieleweke
 
Kama vile wafanyavyo wachungaji wa dini zetu za kikristo na masheikh kukataa ngome za muovu ibilisi basi hivyo hivyo waikatae na kuvunja ngome zote za CCM. CDM hoyeeeeeee.
 
Ni tamko lililojaa ukweli ingawa kuna maneno makali kiasi na hii inaonesha ni jinsi gani watu walivyochoka na jeshi la Polisi kiasi kwamba hakuna mwenye imani tena na jeshi hili.
Hii ni nchi yetu sote na inatakiwa kila mmmoja wetu afuate sheria,si sheria itumike kwa mmoja huku kwa mwingine kuwe na visingizio kuwa usifanye mambo kwa kufuata mwenzio alifanya kama wewe,kauli kama hizi ndio huleta machafuko kwani zinaonekana kuegemea upande mmoja na hazina usawa.
Natambua baada ya tamko hili inawezekana kabisa huyu mwenyekiti akakamatwa na kufunguliwa mashitaka ya uchochezi ila hata siku moja hawawezi kurudisha nyuma harakati za wapenda haki na maendeleo ya nchi hii ambao wanajitolea kila siku kuhakikisha nchi hii inatawaliwa kwa misingi ya usawa na kila mtu anapata haki sawa na hakuna matabaka.
Bila maneno makali hawaelewei hao, vichwa ngumi sana na ni kama watoto yaanu masikio yao wameyahamishia kwenye makalio aka masabuli na ili wasikie mpaka utumie kiboko.
 
Naam..............
Utumwa noooooo..haki daimaaaaaaaa.Ccm jitafakarini,kuna siku kila mmoja atasimama kutoa hesabu ya mema na mabaya..nasema jitafakarini .bei ya dola leo ni 1745-1850...Uchumi wa TZ umekumbwa na nini???.wahusika hawaonii??,haya yote ni kutokana na kutoheshimu haki ya mtanzania..

Kuanguka kwa uchumi wa Tanzania kunatokana kwanza Serikali imeruhusu kutumika kwa Dola ya marekani ndani ya nchi kwa huduma mabali mbali ambazo zingeweza kufanyika kwa shilingi,mfano shule nyingi sasa wanalipa Ada kwa Dola,Dstv Dola unaporuhusu fedha za nje zitumike ndani maana yake unaua thamani ya pesa yako mwenye,Hakuna anaestuka wala kujali hali hii kwa vile waliopewa dhamana ya kuongoza nchi wametawaliwa na tamaa ya utajiri,pia uwepo wa raia wanje kufanya kazi za wazalendo malipo yanafanywa kwenye nchi walizotoka unategemea nini NAICHUKIA CCM,YENYE WATU WAVIVU KUFIKIRI NA KUAMUA.
 
Tupo pamoja makamanda wa SINGAPORE, ni lazima tupande nao juu kwa juu mpaka magamba yasalimu amri.............. siku zao zinahesabika kawni hata police wenyewe wameshachoka kukesha kwa ajili ya magamba
 
nguvu yenu ni kubwa hata zaidi ya mnavyoidhania. Tafadhali msirudi nyuma
 
Mapambazuko Libya yalianzia Bengazi (TZ ni Arusha) yakapita miji mingi ikiwa ni pamoja na Tripoli (DSM) na kuishia Sirte (Bagamoyo). Nadhani ndiko tunakoelekea.
 
Hasira zinazidi kujaa vifuani mwa watu! Hatari inaongezeka na sioni mwenye busara kujitokeza kujaribu kuinusuru nchi! Haki tunablast!
 
IGP Said Mwema alipokamatwa Lema uliuliza ana kosa gani? Uliuliza kwanini vijana wa CCM hawakukamatwa? Ulituma Kamanda Sirro na Mwenzake toka Makao Makuu kwenda Arusha kutafuta nini? Uliwalipa kwa pesa ya jamuhuri ipi? wanatumikia watanzania au vigogo fulani wanaovaa magwanda ya kijani? Ulitafuta suluhu? Na Hakimu wa Mahakama ya Arusha, Kama dhamana ya Lema ilikuwa wazi imekuwaje Jumatatu mkakataa kumtoa? Mkuu wa Mkoa Arusha alienda kufanya nini alfajiri mahakamani? Je ni ratiba yake ya kila siku? kama sio hivyo kwanini siku hiyo tu? Je kesi ya Lema ilitajwa tena bila yeye kuwepo? kama haikutajwa nani alifunga dhamana kwa wiki hii na kusema iwe wazi wiki ijayo? kwanini?. Je wakati UVCCM wanafanya mikutano bila kibali Arusha jeshi lilikuwa likizo? Kama halikuwa likizo kwani hao hawakukamatwa? Jeshi la Polisi mlitumia toleo lipi la sheria kuwaacha UVCCM? Toleo hilo lilibadilishwa lini ili kuhalalisha kumkata Lema, Mbowe, Slaa na Lissu? Je Mlipobadili mliwapa taarifa? Mlitumia kigezo gani kubadili matumizi ya sheria? IGP Kumbuka katika tukio la Arusha CHADEMA walitangaza mkutano Jiji lote, kwa gharama za vipeperushi, magari, vipaza sauti na hata Redio, ulishauriwa ukakurupuka kuahirisha jioni kwa televisheni bila kujali ni Watanzania wangapi wanaangalia TV? Barua mbili zilizotoka ofisi ya OCD na RPC Arusha zote zinapingana. Je kuna majeshi mangapi nchini? Kuna kitu mmechemsha mtake msitake. OMBENI RADHI KUREJESHA AMANI YA ARUSHA
 
Back
Top Bottom