TAMKO CUF: China msiwe adui wa demokrasia Tanzania kwa maslahi yenu

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
20,229
23,916
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
01 April 2016

CHINA MSIWE ADUI WA DEMOKRASIA TANZANIA KWA MASLAHI YENU

Nchi ya China jana kupitia balozi wake Dk.Lu Youqing alipokuwa anazungumza na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Raisi Muungano na mazingira January Makamba alikaririwa na vyombo vya habari akisema China inaamini uchaguzi uliofanyika hivi karibuni Zanzibar ulikuwa huru na haki.

Chama cha wanachi CUF tunaelewa kwamba kwa nchi yeyote inayofahamu Demokrasia, Uhuru na Haki ni nini hawezi kuasema uchaguzi wa marudio Zanzibar ni wa huru na haki. Ama kama nchi hiyo itaamini kwa haki na uhuru huo wa ZEC ya Jecha basi nchi hiyo sana ya Kidemokrasia nchini mwake. CUF hatuamini kwamba China haijui demokrasia ikoje ila wanahalalisha uchaguzi haramu wa Marudio Zanzibar kwa sababu ya maslahi yao ya kiuchumi kwa raia wa China nchini Tanzania na huko kwao China.

Chama kikongwe kinachotawala China CCP na kile chama tawala Tanzania CCM wamekuwa na uswahba wa muda mrefu.

Uswahiba huu umefanya China kuwa kipofu kuhusu mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binnadamu na ukiukwaji wa demokrasia wakihofia kuharibu uswahiba wao na CCM.

Uswahiba ambao unamaslahi zaidi kwa China kuliko Tanzania, ndio maana
wako tayari kuhalalisha haramu kuwa halali.

China inaamua kuunga mkono kukandamizwa kwa demokrasia nchini Tanzania ili kujikomba kwa serikali ya CCM waendelee kupata hisani zaidi kwa masalhi ya taifa lao bila kujali CCM kwa kiasi gani inakuwa katili kwa
watanzania.

Tumekuwa tukijaribu kuchunguza baadhi ya mambo ambayo yakihusisha
wachina hapa nchini na kutilia shaka sana urafiki wa China wa Tanzania labda ni wakinafiki zaidi na kudalali maliasili za watanzania.

China inapata tenda kubwa za ujenzi nchini Tanzania mfano ujenzi wa barabara ambazo nyingine zishaanza kuharibika,madaraja na majengo makubwa nchini.Hata mradi wa kusafirisha gesi wamo pia.

Tanzania kumekuwa na ongezeko la wachina wakifanya biashara
zainazofanywa na watazania kama vile kuuza maua kariakoo,yeboye bo na sehemu mblimbali nchini.

Jambo hili limekuwa likitia wasiwasi sana hasa ukiuliza hawa ndio wawekezaji waliokuja kuuza maua na yeboyebo.

Swali hili serikali imekuwa ikishikwa nakigugumizi namna ya kujibu.

Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya mauajia ya tembo .

Changamoto ambayo raia wa China wamekuwa wakishukiwa kuhusika.

Mfano Novemba 2013 maeneo ya Mikocheni Dar es Salaam, wachina watatu walikamatwa na vipande mia saba 700 vya meno ya tembo.
Tanzania inakabiliwa na chanagamoto ya bidhaa feki kutoka China. CUF tumekuwa tukihoji ni kwa nini serikali imeshindwa kuzuia bidhaa hizi
feki kutoka China a mpaka leo hii bado zipo na zinaadhiri uchumi.

Chombo cha kudhibiti ubora wa bidhaa nchini TBS kipo na bidhaa feki kutoka China zipo.

Raia kutoka china wamekuwa wakiongezeka sana nchini na mara kadhaa baadhi yao wamekuwa wakikamatwa kwa kuishi nchini bila kufuata utaratibu.

Chama cha wananchi CUF tunaionya sana China iache siasa kufumbia macho ukiukwaji wa demokrasia nchini kwa maslahi yao na kuitumia Tanzania kujinufasha na rasilimali zilizopo bila kujali amani itakapovunjika hapo baadae.

Pia tunaitaka serikali kwa makini sana iangaliae mahusiano na misaada inayotolewa na China inamalengo gani yaliyofichika kwa Taifa letu.

HAKI SAWA KWA WOTE
Mh.Abdalah Mtolea( MB)
Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya
Nje CUF Taifa
075881111.
 
Washolisiti hao wana lundo la majeshi lkn hawajui vita, Tanzania ina jeshi bora kuliko China, hawanaga sauti duniani
 
Mtu hana hicho kiitwacha 'demokeasia' kwao ata kihubirije kwa watu???.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
01 April 2016
CHINA MSIWE ADUI WA
DEMOKRASIA TANZANIA KWA
MASLAHI YENU
Nchi ya China jana kupitia balozi
wake Dk.Lu Youqing alipokuwa
anazungumza na waziri wa nchi
ofisi ya makamu wa Raisi
Muungno na mazingira January
Makamba alikaririwa na vyombo
vya habari akisema China inaamini
uchaguzi uliofanyika hivi karibuni
Zanzibar ulikuwa huru na haki.
Chama cha wanachi CUF
tunaelewa kwamba kwa nchi
yeyeto inayofahamu
Demokrasia,Uhuru na Haki ni nini
hawezi kuasema uchaguzi wa
marudio Zanzibar ni wa huru na
haki.Ama kama nchi hiyo itaamini
kwa haki na uhuru huo wa ZEC ya
Jecha basi nchi hiyo inamatatatizo
sana ya Kidemokrasia nchini
mwake.
CUF hatuamini kwamba China
haijui demokrasia ikoje ila
wanahalalisha uchaguzi haramu
wa Marudio Zanzibar kwa sababu
ya maslahi yao ya kiuchumi kwa
raia wa China nchini Tanzania na
huko kwao China.
Chama kikongwe kinachotawala
China CCP na kile chama tawala
Tanzania CCM wamekuwa na
uswahba wa muda
mrefu.Uswahiba huu umefanya
China kuwa kipofu kuhusu mambo
mbalimbali ya ukiukwaji wa haki
za binnadamu na ukiukwaji wa
demokrasia wakihofia kuharibu
uswahiba wao na CCM.Uswahiba
ambao unamaslahi zaidi kwa
China kuliko Tanzania, ndio maana
wako tayari kuhalalisha haramu
kuwa halali.
China inaamua kuungamkono
kukandamizwa kwa demokrasia
nchini Tanzania ili kujikomba kwa
serikali ya CCM waendelee kupata
hisani zaidi kwa masalhi ya taifa
lao bila kujali CCM kwa kiasi gani
inakuwa katili kwa
watanzania.CUF Tumekuwa
tukijaribu kuchunguza baadhi ya
mambo ambayo yakihusisha
wachina hapa nchini na kutilia
shaka sana urafiki wa China wa
Tanzania labda ni wakinafiki zaidi
na kudalali maliasili za
watanzania.
China inapata tenda kubwa za
ujenzi nchini Tanzania mfano
ujenzi wa barabara ambazo
nyingine zishaanza
kuharibika,madaraja na majengo
makubwa nchini.Hata mradi wa
kusafirisha gesi wamo pia.
Tanzania kumekuwa na ongezeko
la wachina wakifanya biashara
zainazofanywa na watazania kama
vile kuuza maua kariakoo,yeboye
bo na sehemu mblimbali
nchini.Jambo hili limekuwa likitia
wasiwasi sana hasa ukiuliza hawa
ndio wawekezaji waliokuja kuuza
maua na yeboyebo.Swali hili
serikali imekuwa ikishikwa
nakigugumizi namna ya kujibu.
Tanzania inakabiliwa na
changamoto kubwa ya mauajia ya
tembo .Changamoto amabayo raia
wa China wamekuwa wakishukiwa
kuhusika.Mfano Novemba 2013
maeneo ya Mikocheni Dar es
Salaam,wachina watatu
walikamatwa na vipande mia saba
700 vya meno ya tembo.
Tanzania inakabiliwa na
chanagamoto ya bidhaa feki
kutoka China.CUF tumekuwa
tukihoji ni kwa nini serikli
imeshindwa kuzuia bidhaa hizi
feki kutoka China a mpaka leo hii
bado zipo na zinaadhiri
uchumi.Chombo cha kudhibiti
ubora wa bidhaa nchi TBS kipo n
bidhaa feki kutoka China zipo.
Raia kutoka china wamekuwa
wakiongezeka sana nchini na
mara kadhaa baadhi yao
wamekuwa wakikamatwa kwa
kuishi nchini bila kufuata
utaratibu.
Chama cha wananchi CUF
tunaionya sana China iache siasa
kufumbia macho ukiukwaji wa
demokrasia nchini kwa maslahi
yao na kuitumia Tanzania
kujinufasha na rasilimali zilizopo
bila kujali amani itakapovunjika
hapo baadae.Pia tunaitaka serikali
kw makini sana iangaliae
mahusiano na misaada
inayotolewa na China inamalengo
gani yaliyofichika kwa Taifa letu.
HAKI SAWA KWA WOTE
Mh.Abdalah Mtolea( MB)
Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya
Nje CUF Taifa
0758811110.


Najuta kuzaliwa nchi yenye wajinga wengi
 
Hawa wavimba macho watuachie mambo ya nchi yetu wenyewe.
China wamegeuza Tz shamba la malighafi na dampo la bidhaa zao fake.
Siku upinzani wakichukua nchi Wachina ni jipu la kwanza kutumbuliwa.
Teh Teh ...@nifah habari yako?
 
Waseme nchi haifanyi mambo kwa demokrasia wakale wapi? waka dump wapi bidhaa zao za chini ya kiwango? Mpaka tembo watakapo isha na wao kutohitaji kitu toka Afrika ndipo watakapo kosoa utendaji wa nchi hii, vinginevyo lazima watupake mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Wazee wa salnag hao boda boda.com

Sawa ni ajira lakini wanatuumiza simu zitakazo zimwa mwezi wa6 zote ni za kichina

wachina wabaya mpaka wameshawatia hasara watz na bado munawakumbatia.
 
Meno ya tembo,simu mbovu,kujazana Tanzania,kupokonya wenyeji viwanja,ujenzi wa barabara mbovu nk.Watakula wapi hawa lazima watahalalisha haramu ili waendelee kuuwa tembo.Mijangili hii.
 
Taifa la Wajanja wajanja! Hawa Jamaa Na Mkwere walikua bega mwa bega sana! Naona Jamaa nae anazidi kuyajenga nao!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom