ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 628
- 1,561
CHAMA cha ACT Wazalendo kinalaani vikali uamuzi wa jeshi la polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa uliotangazwa leo na Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo Nsato M Msanzya-CP.
Ikumbukwe kuwa uamuzi huu wa jeshi la Polisi unafuatia kuzinduliwa kwa “Operesheni Linda Demokrasia” baada ya Wabunge saba wa vyama vya upinzani kusimamishwa Bungeni baada ya kupinga Kitendo cha Serikali kuzuia kurushwa kwa matangazo ya Bunge moja kwa moja.
Mikutano ya “Operesheni Linda Demokrasia” inayoratibiwa na Chama chetu ilipangwa kufanyika kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya na Morogoro. Hadi sasa umeshafanyika mkutano mmoja jijini Dar es Salaam.
Pia Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto ameitwa Polisi kituo cha Kati leo tarehe 7/6/2016. Ndugu Zitto ameitwa na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar Es salaam Bwana. Wambura. Ameomba asiende leo kwa kuwa ni karibu na masaa ya kufuturu. Atakwenda kesho saa tatu asubuhi.
Chama chetu kinapinga vikali uamuzi huu wa jeshi la polisi kwa sababu hauna mashiko kwa kuwa haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano ni ya kisheria kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 (kifungu cha 11(1)
Uamuzi huu wa Jeshi la Polisi unavunja haki ya raia kutoa maoni (Ibara ya 18(a) na uhuru wa kukusanyika (Ibara ya 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sababu iliyotolewa na Jeshi la Polisi kuwa mikutano hii inalenga kuchochea wananchi kutotii sheria ni mwendelezo wa visingizio vya serikali vinavyolenga kuminya uhuru wa wananchi kuikosoa serikali na sasa Jeshi la Polisi limejiingiza katika kuisaidia serikali kutimiza matakwa yake ya ukandamizaji wa Demokrasia unaofanywa ndani na nje ya Bunge
Chama cha ACT-Wazalendo kinawasiliana na wanasheria wetu ili kupata tafsiri ya kimahakama ya uhalali wa jeshi la polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ambayo inatambuliwa na kulindwa na katiba.
Tunalikumbusha Jeshi la Polisi na serikali kwa ujumla kuwa hila hii ya kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani kamwe haitazuia nia njema tuliyonayo wala kushusha ari yetu ya kuitetea na kuilinda misingi ya demokrasia inapokandamizwa na serikali.
Ado Shaibu,
Katibu Itikadi, Mawasiliano na Uenezi
ACT Wazalendo
Imetolewa leo tarehe 07 Juni 2016