msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 839
- 1,472
Prof. Shemdoe ambaye ni katibu mkuu ofisi ya Rais-TAMISEMI amesema tokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipoielekeza Ofisi hiyo kufanya mchakato wa kuajiri walimu 6,000 ili kufidia baadhi ya watumishi hao kwa sababu mbali mbali, kumezuka wimbi la matapeli na wengine kuwadanganya watu wanaoomba ajira kwamba watawasaidia kupata ajira hizo.
“Nimepata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa, wapo baadhi ya watu kwa nia ovu wamekuwa wakiwatapeli kwa kuwaomba fedha baadhi ya walimu wanaotaka kuomba ajira na kuwataka watoe pesa ili zifikishwe Wizarani kwa ajili ya kuwapatia ajira, nipende kusema wazi kwamba jambo hili halipo,” amesema Prof. Shemdoe.
Prof. Shemdoe na kuongeza kwamba, vishoka wote watakaobainika kutekeleza utapeli huo watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya dola, huku akiwataka wale wote watakaokumbana na adha hiyo kutosita kutoa taarifa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Pamoja na kauli za vitisho alizotoa Prof. Shemdoe, ukweli ni kwamba ofisi anayoiongoza ndio chanzo cha utapeli huo kwa sababu tangu Rais atoe tamko la kuajiri walimu 6000 kwa haraka ili kuziba nafasi za walimu waliostaafu, kufariki au kuacha kazi, wizara iko kimya haijatolea ufafanuzi wowote kuhusiana na ajira hizo.
Mtakumbuka mwezi September aliyekuwa Rais kwa wakati huo, hayati JPM alipotangaza kibali cha kuajiri walimu elfu 13 jioni yake aliyekuwa waziri wa TAMISEMI kwa wakati huo Bw. Suleiman jaffo alijitokeza na kutangazia umma siku dirisha la maombi litakapofunguliwa ili walimu waweze kutuma maombi yao na kweli ikawa hivyo.
Lakini cha kushangaza tangu mhe. Samia Suluhu atoe tamko la kuajiri walimu 6000 siku ya tarehe 6/4/2021 hadi sasa hakuna utaratibu wowote umetolewa kuhusiana na ajira hizo, si katibu mkuu au waziri Ummy Mwalimu wote wako kimya.
Kitendo cha waziri na katibu wake kuwa kimya ndio kimepelekea kuibuka kwa utapeli kwa sababu mpaka sasa waombaji hawajui utaratibu utakaotumika kama wataajiriwa kwa kutumia majina yalipo kwenye database au dirisha la maombi litafunguliwa upya.
Sasa basi ili kukomesha tabia hii ya kitapeli ni muda muafaka waziri Ummy Mwalimu na katibu wake prof. Shemdoe wajitokeze hadharani kutoa utaratibu utakaotumika kwenye hizi ajira. Kama dirisha linafunguliwa upya waeleze wazi ni lini litafunguliwa ili kuwaondoa hofu waombaji na kuwaepusha kurubuniwa na matapeli.
Nawasilisha kwenu ma-GT