Tambua Mambo sita kuhusu Halloween

Tambua Mambo sita kuhusu Halloween

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,148
Reaction score
10,571
Habari za alhamis yenu natumaini mpo salama. Naomba nilete Uzi huu kuhusu mambo sita kuhusu Halloween au sherehe za Halloween.
Karibuni:
Halloween ni nini haswa? Hii ni muunganiko wa sherehe zinazofanywa hasa katika nchi za Ulaya pamoja na America. Ni moja kati ya sherehe za ajabu kidogo dunia kwani inajumuisha mpaka imani za baadhi ya madhehebu ya kikristo pamoja na kipagani. Ijapokuwa dunia imepiga hatua lakini Halloween imebaki na matendo Yale Yale kwa maana matendo kwenye sherehe za miaka 1700 basi mpaka Leo hufanywa kwa mtindo huo huo. Humu ndo watoto huvaa vinyango kama mizimu pamoja na mashetani. Pia nguo zenye alama kama mifupa ya binadamu na majini.
5bad44852400003000961216.jpeg
Halloween Costumes

Lakini je Halloween ilitokea vipi? Na ilitokea wapi na kwanini sikukuu hii imechukua sehemu za maisha ya binadamu?
Sikukuu hii haikuanzishwa na Yesu wala mitume wake. Pia haijaanzishwa na Biblia kwa namna yoyote ile. Soma kitabu cha Mathayo 16: 13-17.


1. Halloween ni sikukuu iliyoanzishwa na Waceltic.

Zaidi ya miaka 2000 iliyopita, Jamii hii ilianzisha mtindo wa sherehe kwa mgongo wa sherehe za mavuno kila tarehe ya 31 mwezi oktoba. Waliamini kuwa usiku Wa tarehe hiyo roho chafu za wafu hurudi duniani kwa ajili ya kuharibu mazao pamoja na kuwaingilia watu. Kitu pekee walichokifanya ilikuwa ni kuvaa kama mfano Wa mizimu pamoja na sura za kutisha Ili kuzichanganya roho hizo.

2. Ni sikukuu iliyoongezea nakshi na Waroma.

Katikati ya mwaka 43 A.D baada ya Yesu jamii ya Celtic ilichukuliwa na utawala Wa Roma na hivyo Waroma kuamua kuifanya Samhain siku hi iwe bora zaidi kwa kuingiza na kuwa mchanganyiko Wa sikukuu mbili za kiroma. Moja ya sikukuu ilikuwa ni Feralia ambayo ilikuwa ni sikukuu yq kuwakumbuka wafu pamoja na sikukuu ya Pomona ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya kumbukumbu ya mungu mwanamke ambaye alitumia Tufaha kama alama take. Ilichukua miaka kumi kwa watu kuanza kusherekea sikukuu tatu na kuziita Halloween.

3. Asili ya neno Halloween.

Mwaka Wa 609 A.D wakatoliki walitaka kuwepo na matendo yenye kuamsha hisia wakati Wa kusherekea. Na ilipelekea Papa Boniface kutengeneza sikukuu iliyoitwa Sikukuu ya watakatifu wote. Iliyosherekewa kila tarehe 1 mwezi Wa Novemba. Hii ilikchukua asilimia kubwa ya vitu vinavyofanywa kwenye ile sikukuu ya waceltic ya Samhain. Sababu kuu ya kufanya hivi ilikuwa ni kuwavutia wapagani Wa Celtic kuingia kwenye ukatoliki. Neno Halloween limetokana na neno Alholowmeesse ama Sikukuu ya Watakatifu wote.
images%20(8).jpeg
pumpkin.

4. Ilikuwa ngumu sana kwa Waamerika kukubali sikukuu hii.

Mwanzoni Wa miaka ya 1800 ndo wamamerika walipoanza kuingiza tamaduni za sherehe hii.
Lakini mara baada ya kuingia kwa machotara wa kiirish pmoja na Celtic ndo wakaanza kuingia tamafuni hizo mdogo mdogo. Kisha wakaanza kuvaa vinyango pamoja na kuiga mitembeo ya majini na mapepo.
images%20(10).jpeg
sherehe imepamba moto.

5. Je wajua kuwa Halloween ni sikukuu ya pili kwa umarufu na ukubwa ndani ya marekani?

Ndio baada ya Christmas basi Halloween ndo yenye ufuasi mkubwa ndani ya nchi ya Trump. Lakini sherehe hii ilipoteza utamu katika miaka ya 1920 na 1930, kwani wahuni walitumia kuvunja nyumba za watu na kuiba kwa kutumia mwamvuli Wa Halloween. Kuanzia miaka ya 1950 watu walitilia mkazo sherehe hii kwa watoto wadogo hasa hasa. Hivyo kupelekea kupendwa na Wazazi pamoja na watoto wao.
images%20(12).jpeg
watu wakiwa wanasherekea sikukuu hii.

6. Zaidi ya shilingi dola bilioni 4 za kimarekani zinatumika kwenye sherehe hizi.

Ndio Halloween huchukua kiasi hiki katika maandalizi yake ikiwemo mapambo, pamoja na shamrashamra za tukio hili. Sekta ya utengenezaji Wa Pipi pamoja na Chocolate hutengeneza dola za kimarekani bilioni 2 tu hivyo kupelekea robo ya pato la taifa kwa mwaka tu.
images%20(11).jpeg
watoto wakiwa na furaha.

Ni hayo tu kwa sasa. Mambo ni mengi Sana kuhusu hii sikukuu ila nimeleta mmbo sita tu kwanza ili kuonyesha ni nini haswa hufanyika kwa wenzetu.
Karibuni kuchangia na kuuliza chochote kuhusu Halloween.
I stand to be corrected anywhere.
Asanteni
Cc. @Mshana_Jr @Malcom_Lumumba zuri na wengine
 

Attachments

  • Jack-o'-Lantern_2003-10-31.jpeg
    Jack-o'-Lantern_2003-10-31.jpeg
    38.6 KB · Views: 32
  • Thanks
Reactions: Qwy
Asante sana mkuu, nimeona sana kwenye movies ila nilikua sijawahi kuielewa hii sikukuu.
 
Asante sana mkuu, nimeona sana kwenye movies ila nilikua sijawahi kuielewa hii sikukuu.
Wanapenda sana kuweka kwenye movies mkuu
 
Back
Top Bottom