yegella
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 3,113
- 1,104
na Abdallah Khamis
AHADI ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula, kuwaengue viongozi walioshinda kwa rushwa ndani ya chama ndani ya miezi sita imeota mbawa.
Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa chama kuwaruhusu baadhi ya waliokuwa wakituhumiwa kugombea nafasi hizo kwa mara ya pili na kushinda baada ya kutengua matokeo ya awali.
Ikiwa imepita miezi kumi sasa tangu Mangula atangaze mkakati huo, hakuna mshindi aliyeondolewa katika nafasi yake kwa tuhuma za rushwa zaidi ya wale waliotuhumiwa kupewa nafasi ya kurudia uchaguzi.
Wakati baadhi ya watuhumiwa wakirejea katika nafasi zao katika uchaguzi uliofanyika kimya kimya mwezi uliopita, Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliliambia gazeti hili kuwa hakuna kiongozi aliyepatikana na hatia ya rushwa.
Kwa mujibu wa Nape, makamu mwenyekiti wao ameomba miezi sita zaidi kuweza kukamilisha kazi hiyo.
Miongoni mwa watu waliorejea katika uchaguzi na kushinda ni Mbunge wa Mchinga, Said Mtanda na Mbunge wa Longido, Lekule Laizer, waliokuwa wameshinda ujumbe wa NEC Taifa kupitia wilaya zao.
Mtanda alidaiwa kutoa rushwa, kupendelewa katika uchaguzi huo pamoja na kura zilizomuingiza kutokufika nusu ya kura za wajumbe wote waliopiga kura.
Lazier alikanusha kuhusishwa na tuhuma za rushwa na kueleza kuwa alilalamikiwa kwa kupata kura zilizokuwa chini ya nusu ya wapiga kura.
Akizungumza na Tanzania Daima, Mtanda alisema hakutoa rushwa katika uchaguzi wa awali licha ya Kamati Kuu ya CCM kuamua kurejea uchaguzi wa nafasi yake.
Alisema kilichosababisha uchaguzi huo kurudiwa ni baada ya kubainika kuwa kura za awali zilikuwa hazijafika nusu ya idadi ya mara mbili ya mshindani aliyemfuatia.
Mtanda aliongeza kuwa licha ya kushinda katika uchaguzi wa marudio alibaini kuwa zilikuwa ni kelele na mbinu alizoziita chafu kutoka kwa wapinzani wake wa kisiasa.
Naye Laizer alisema kuwa mshindi alitakiwa kupata kura zaidi ya nusu ya washindani wake, kwamba hilo la rushwa hajahusishwa nalo.
Chanzo: Tanzania Daima