Deejay eXii
Member
- Feb 22, 2025
- 40
- 44
_____________
▪️ Genre: War, Action, Drama
▪️ Date: April 20, 2023
▪️ Rate: 7.5/10 IMDb
▪️ Time: 2h 3m
▪️ Director: Guy Ritchie
▪️ Main characters:
Jake Gyllenhaal kama Sgt. John Kinley
Dar Salim kama Ahmed (mkalimani)
_____________
SHORT STORY BEHIND
Story hii si ngeni mjini...!, Eh ndivyo wasemavyo 'Gen Z'. Nami nakwambia hii si Stories za madenge wa jarida la 'Sani' bali ni true event.
Mnamo novemba 11, 2001, magaidi wa Al-Qaeda (chini ya uongozi wa Osama bin Laden) walitekeleza mashambulizi ya kigaidi ndani ya ardhi ya Marekani. Ndege nne za abiria zilitekwa. Mbili ziligonga World Trade Center (Twin Towers), moja Pentagon, na ya nne ikaangushwa Pennsylvania kwa juhudi za jeshi la marekani kabla ya kufikia ilikokuwa target ya shambulio lake.
Zaidi ya watu 3,000 walikufa. Hili liliwasha moto wa hasira ya Marekani. Kutokana na nguvu ya ushawishi alokuwa nayo marekani ndani ya Baraza la umoja wa usalama kwa nchi za NATO baada ya mashambulizi ya awali, Marekani iliishinikiza NATO kuanzisha jeshi la ISAF, kusaidia kukomesha waasi, kutoa misaada, na kufundisha jeshi la Afghanistan.
ISAF halikuwa jeshi la Marekani pekee. Lilikuwa ni muunganiko wa majeshi ya mataifa mbalimbali yaliyojiunga kusaidia serikali ya Afghanistan kudhibiti usalama wake, kuwaondoa Taliban, na kuandaa mazingira ya utawala bora. Majeshi ya nchi kama Marekani, UK, Ujerumani, Ufaransa, hata nchi kama Jordan na Georgia; walikuwa ndani ya mpango huo wa ISAF.
Sasa wakati mambo hayo yakiendelea Osama alikuwa Afghanistan. Alikuwa analindwa na serikali ya Taliban, ambayo ilikuwa inatawala sehemu kubwa ya nchi hiyo.
Hapa nataka uelewe vizuri kabla ya kuendelea na tambara letu.
Kwa wakati huo, Afghanistan haikuwa na utawala wa kiraia unaotambulika kimataifa. Badala yake, ilikuwa chini ya utawala wa Serikali ya Taliban (1996–2001). Taliban walichukua madaraka mwaka 1996, baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mingi tangu kuanguka kwa serikali iliyokuwa ikisaidiwa na Muungano wa Kisovyeti. Kufikia 2001, Taliban walikuwa wanatawala karibu 90–95% ya nchi nzima japokuwa Serikali yao haikutambuliwa rasmi kimataifa (ni nchi tatu tu Pakistan, Saudi Arabia, na UAE, ndizo zilizowatambua)
Sasa tuendelee...!
Marekani ikatoa masharti kwa Taliban, "Tukabidhini Osama bin Laden au tutachukua hatua za kijeshi.”wao Taliban wakakataa na ndipo sasa Marekani na washirika wengine waliamua kuivamia Afghanistan rasmi mnamo Oktoba 7, 2001 chini ya operesheni ya kijeshi iitwayo, "Operation Enduring Freedom (OEF)" wakidhamiria Kujenga upya Afghanistan kuleta demokrasia, usalama, na kupunguza tishio la ugaidi duniani.
Ni muhimu kujua historia kabla ya kutizama hizi Filamu za kivita ili usijekuwa unatazama tu na hauelewi unatizama nini. Tuianze sasa Filamu yetu namna hii.
Tukiwa Kandahar ndani ya Base ya kijeshi ya Marekani kaskazini mashariki mwa nchi ya Afghanistan. Sgt. John Kinley alikuwa akiongoza kikosi maalum cha wanajeshi wa Marekani waliokuwa wakifanya kazi ya "Intelligence Reconnaissance & Taliban Supply Chain Interdiction", Kwa Kiswahili tunasema;
"Operesheni ya kijasusi ya kuvuruga mnyororo wa usambazaji wa silaha wa Taliban." Lengo kuu likiwa ni kujaribu, kutambua mahali ambapo Taliban walikuwa wanajificha na pili kufuatilia vyanzo vya silaha, vifaa, na taarifa za kijasusi.
Hii ikawatibua Taliban na kuchukizwa jinsi ambavyo Marekani ilikuwa ikijipenyeza kwa raia wao na kuteka imani ya wa-Afghanistan na kuuza taarifa zao muhimu. Moto ukawaka.
Awali John kinley hakuwa anamwamini Ahmed(mkalimani katika kikosi alichokuwa akikiongoza Sgt John). Ila Ahmed hakuwa tu mkalimani bali alikuwa ni ex- smuggler. Mhuni na mtoto wa mjini yaani tunaweza kusema alikuwa anazijua kona zote za Kandahar na alikuwa anawajua wataliban vizuri tu. Wakiwa katika Doria zao za kila siku, jamaa wakatia maguu kwenye mgodi mdogo uliokuwa zaidi ya kilomita 100 toka ilipo Base yao.
Kama John kinley na kikosi chake wangejua watakachokutana nacho hapo mgodini labda wasingefika kabisa hapo maana show waliyokutana nayo ilimfanya Kinley kukata tamaa ya kuishi, kuamini, na kuuona ubinadamu na zaidi kubakisha agano lake juu ya Ahmed na familia yake. Nimekuchanganya eeh...!?, Sasa katizame hili dubwana ndo utanielewa.
Hili dude hutakiwi kupepesa macho wala kumeza mate. Cha kufanya we andaa tu popcorn za laki 😁. Mi najikataa zangu tukutane kwenye TAMBARA lingine.
#Dj_eXii