CLEVER SQUIRREL
Senior Member
- Feb 20, 2019
- 121
- 117
Natumaini wana Jf weekend imeanza salama.
Naomba tueleweshane kwenye mambo haya:
1.Unakuta mtu kwa mwezi amechangia watu sita michango ya harusi hapo mshahara wake ni 650,000 unajiuliza huu uwezo unatokea wapi? Kufatilia kumbe kakopa vikoba. Yaani kila mwezi mtu anachanga harusi zaidi ya tatu,nne,tano ukiangalia maisha ya nyumbani kwake utaona huruma. Kama mtu anauwezo ni jambo jema lakini wengi uwezo huo haupo. Jamani watanzania tuelewe kuchanga ni hiari kama huna kuwa muwazi.Pia kwa wale wanaooa na kuolewa tujitahidi kuwa halisia ikiwezekana jipangeni hata ndani ya mwaka mzima kwa kuweka pesa taratibu,mtajisikiaje kwenye harusi yenu mmesimamia shoo ya kila kitu mkawaambia wageni waalikwa waje na chupa za wine tu?Linawezekana.Watu wakimaliza harusi unakuta wana madeni chungu mzima.
Natamani kuona harusi zetu zikiwa nafuu sana.
2.Kumwaga chakula.
Aisee katika vitu inavyoboa hili moja wapo tena hujitokeza sana kwa wale middle income earners wanaoelekea kuwa top earners. Eti mtu umejikakamua umempa mtu offer ya msoc expensive afu anakula nusu eti I'm full! Nyambafu! afu kakishikashika kila kona. Hata kwenye familia zetu nyingi haya yapo.Ni vema kupima kiasi ambacho unauhakika utamaliza.Wazazi tuwe makini na hili. Tukumbuke kuna watu wanalala njaa.
3.Matumizi ya sukari na mafuta ya kupikia.
Naamini watanzania wenzangu wengi mmeelimika na mnajua madhara ya kutumia vitu hivyo kwa kiasi kilichopitiliza.
Bwana we kuna dada mmoja wa kazi nilimpata mkoa mmoja Kanda ya ziwa asubuhi kunywa chai anaweka vijiko vinne vya sukari wanafamilia tukabaki tunashangaana. Katika magonjwa manne yanayoongoza kuua watanzania mojawapo ni kisukari.Nilikuwa naongea na doctor mmoja rafiki yangu akanieleza marekani ilipopitia miaka ya 70 na 80 ndio tulipo sisi.Wenzetu baada ya kujua madhara ya excessive sugar intake wamepambana sana kuelimisha watu kupunguza matumizi ya sukari ingawa bado ni tatizo.
Lakini kina mama na nyie mnalakujibu.
Kuna mgeni mmoja toka uingereza alisema watanzania ni wanywa mafuta,nimeanza kuamini.
Watanzania michemsho na vya kubanika kwetu mwiko.Tunaishia kutokwa vitambi na mashavu tukitikiswa kidogo na malaria tupo hoi.Si lazima kila siku vyakula au mboga vipikwe kwa mafuta au kukaanga mboga kwa mafuta. Unakuta familia ya watu wanne lakini mafuta ya lita tano yanaisha ndani ya siku tano, ni hatariiiiii! Magonjwa ya moyo na Pressure utasikia kila kona unapopita.
Natamani sana watanzania tubadilishe taratibu hizi mbaya.Nilitaka kutiririka zaidi lakini muda haupo upande wangu . Kuna mambo mengine kama manne hivi bado yanatutesa watanzania tayaandika hii weekend.
Ova.
Sent using Jamii Forums mobile app