Tamaa ya Umaarufu Yapelekea Aiage Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamaa ya Umaarufu Yapelekea Aiage Dunia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 24, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwanamke nyota wa filamu za ngono wa nchini Ujerumani ambaye alijipatia umaarufu mkubwa baada ya kushiriki 'Big Brother Germany' amefariki dunia baada ya operesheni ya sita ya kurekebisha matiti yake ili jina lake liendelee kutamba kwenye vyombo vya habari.
  Carolin Berger mwenye umri wa miaka 23 ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na ushiriki wake kwenye mashindano ya "Big Brother Germany", amefariki dunia kutokana na matatizo ya kiafya aliyopata baada ya operesheni ya sita ya kuongeza ukubwa wa matiti yake.

  Carolin ambaye awali alikuwa akishiriki kwenye sinema za ngono akijulikana kwa jina la Cora kabla ya kushiriki kwenye mashindano ya Big Brother alitaka jina lake liendelee kutamba kwenye vyombo vya habari.

  Carolin alifariki juzi muda mfupi baada ya kumalizika kwa operesheni yake ya sita ya kuongeza ukubwa wa matiti yake.

  Carolin aliongeza ukubwa wa matiti yake toka saizi 34F hadi 34G.

  Alikumbwa na mashambulio ya moyo mara mbili, presha ilishuka ghafla na ubongo wake ulipata madhara makubwa na mwishoe aliiaga dunia.

  Daktari aliyemfanyia operesheni hiyo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

  NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  matukio haya yamezidi sasa bora tumrudie mungu
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  :kev: Allah akbar!!!
   
Loading...