Mashaxizo
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 6,707
- 3,360
Mkuu vipi maswala ya kugawana mali kwenye ndoa ya kiislamu yanakuwaje?
Duh! Baada ya kuachana/kupeana talaka, hakuna kinachobadilika katika mali za wanandoa (mali za mume kwa mume na zile za mke kwa mke/kila mtu na chake) kuhusu mali za pamoja ndio kimbembe kinatokea hapa, kimbembe kingine hutokea ktk kupeana zawadi na masaprais, na ule upenzi wa kumuandikia mkeo mali ktk zile nyaraka. Matatizo haya ndio hufanya kesi kufika mahakamani. Kwa mali iliyochumwa pamoja eg: gari, nyumba, kampuni etc, kadiri ya mtu alivyochangia ndivyo anapata haki yake, tena kunauwezekano mkubwa wa kuuzwa hiyo gari au nyumba. Kwa zile zawadi na masaprais huenda kikamilifu kwa aliezawadiwa. Jina ktk nyaraka vilevile linauzito mkubwa, ukiwa umemuandikia wife/h.b inatambulika hiyo ni yake unless uwe mjanja wa kujitetea. Refers migogoro ya mali hutatuliwa hivi ikifika mahakamani, wanandoa wakikubaliana wenyewe au kwa Mashehe inatosha, lakin jiulize siku hizi tunaachana kwa amani?