Nani haswa anapaswa kutoa talaka kati ya mwanaume na mwanamke?
Na kama wameachana tu je badae mwanaume aeza akadai talaka kwa mwanamke?
Hapo sasa ukitoa na ufafanuzi utakua umetufumbua wengi
Nitoe ufafanuzi hapa maana amu yuko mbali!
Ni hivi, Mume, Mke, Mahakama na hata mashekhe na wakuu wa viviji/mila wanatoa talaka;
MUME: ndie mwenye nguvu zaidi ktk kutoa talaka ie anaweza kutoa talaka hata bila ya kutoa sababu.
Mke: huyu inategemea na dini au kabila, eg: Islam inaruhusu mke kutoa talaka endapo tu atajiskia, sharti alipie fidia flan ivi. Talaka anayotoa mke haina nguvu kiasi kwamba mume akikataa, either mahakama au sheke anatoa iyo talaka. Refers, ikiwa kunasababu za msingi za mke kutoa talaka, sababu hizo mume ndio chanzo eg: hamgegedi, hamuhudumii, anampiga sana nk mke anaweza kuachwa bila fidia.
MAHAKAMA, haiwezi tu kuamua kutoa talaka yenyewe, ni lazi iombwe, na si kila anaeomba talaka, mahakama hutoa talaka.
SHEKHE: hawa ni wakuu wa dini ambao wako qualified kutoa talaka pale inapolazimika eg: mke kaenda kuomba au mume katokomea zaidi ya miezi minne bila kutambulika kaenda wapi na hajaacha maagizo au huduma zozote. Refer hata shekhe wanaweza kuignore kutoa talaka ikiwa hawataridhika na mazingira au sababu.
WAKUU WA VIJIJI/MILA: hutoa talaka kulingana na taratibu za mila zao. REFERS, Mahakama ina nguvu ya kubatilisha talaka yoyote ile.
Nahis nimekusaidia japo kidogo.
Na kama wameachana tu je badae mwanaume aeza akadai talaka kwa mwanamke?
Kwa sisi RC hakuna talaka. ila nilishasikiaga story eti hapa Tanzania Baba mtakatifu (sijui ni yupi sasa) alishawahi kutoa kibali kwa Mahakama kuvunja ndoa fulani. Mwenye kufahamu hiyo story anaweza kuieleza vizuri.Inategemea na imani yako, ktk uislamu mwanaume ndie anayetoa talaka, mwanamke ana haki ya kudai talaka lkn haitoi yeye, kama mume anakua mgumu kuitoa hiyo talaka anaendwa kwa viongozi wa dini kupeleka madai yake,,, sijui kwa dini zingine
Nani haswa anapaswa kutoa talaka kati ya mwanaume na mwanamke?
Mahakama ndiyo inatoa talaka.
Kwa sisi RC hakuna talaka. ila nilishasikiaga story eti hapa Tanzania Baba mtakatifu (sijui ni yupi sasa) alishawahi kutoa kibali kwa Mahakama kuvunja ndoa fulani. Mwenye kufahamu hiyo story anaweza kuieleza vizuri.
Na pia Hakuna mahakama yeyote inaweza kutoa hati ya talaka kwenye ndoa iliyofungwa na kanisa la RC bila kibali cha kutoka Kwenye kanisa. Kwa waislamu hivi inakuwaje wakitaka kupata hati ya talaka ya mahakamani?
Mkuu vipi maswala ya kugawana mali kwenye ndoa ya kiislamu yanakuwaje?Ndoa za kiislamu, huanzia wanandoa wenyewe, ikishindikana wanakwenda kwa Mashehe au mahakama ya kadhi, mtu akikata rufaa inasikilizwa na jaji wa mahakama kuu wakiwemo kadhi. Hii -in law, in facts/practicles kesi za talaka huishia kwa wanandoa, isipokuwa mke amedai talaka mume anakataa, ikiwa hivi mzunguko unakuwa mkubwa kama nilivyoelezea mwanzo.
Refers ndoa iliyofungwa kiislamu talaka yake hutolewa kiislamu majaji wa mahakama kuu just wanasimamia na kuhakikisha sio tu haki itendeke bali ionekane ikitendeka (justice not only done but it manifestly seen to be done)