Talaka za ajabu hapa duniani

Talaka za ajabu hapa duniani

Texas Tom.

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2013
Posts
510
Reaction score
273
1. Jamaa ampa talaka mkewe kwa kuonyesha aibu kubwa na kugomea unyumba kwa mwaka mzima
Mahakama moja huko Tainan (Taiwan huko) ilikubali maombi ya bw. Chen 38 kumlima talaka bi. Lin 29 (wote walimu) baada ya kuwa aibu ya hali juu na kugoma kabisa kutoa unyumba na wakati wa kulala alikua akivaa magauni marefu na muda wote alikumbati mto kwa nguvu kwa zaidi ya mwaka.

Awali washenga na wapatanishi walisisitiza Lin akubali kutoa mambo ila yeye alisaini mkataba wa kukutana kimwili pale tu wanapohitaji kupata mtoto halafu walale vitanda tofauti. Ndipo Chen alipokimbilia mahakamani na mahakama kuamuru Lin kumlipa Chen dola za kitaiwan 300,000 alizonunulia nyumba (inaelekea hapa Chen hakua na mpango wa kununua nyumba wakati wa ukapera) na kurudisha mahari kwa familia ya Chen

2.Mwanamke aomba talaka baada mumewe kujaribu kuchungulia na kutaka kuona uso wa mkewe baada miaka 30 ya ndoa
Mwanamke wa Saudia Arabia aliomba talaka mwaka 2008 baada ya mumewe kutaka kuona uso wa mkewe.(Ngoja niulize kwanza..hivi tunapotongoza, tunatongoza watu tusiowaona usoni?) Wanandoa hao waliishi kwa miaka 30 bila ya mumewe kuuona uso wa mkewe. Mke wake huyo mwenye aliekua na umri wa miaka 50 aliishi maisha ya kufuata utamaduni wa asili wa kijijini kwao kusini mashariki karibu na mji wa Khamis Mushayt wa kuficha uso wake wakati wote.

Usiku mmoja mume wake huyo alikuja na kujaribu kuinu kitambaa (veil) wakati mkewe kalala ili kuuona uso wa mkewe ghafla mke kashtuka na aliomba talaka papo hapo na ilikua ni kosa lisilopewa nafasi ya kusamehewa japokuwa mwanaume kaomba sana msamaha lakini talaka ilitoka.


3.Mwanamke aomba talaka baada kasuku kurudiarudia maneno ya "Nakupenda" na "Kuwa na Subira"
Mwaka 2001 huko China mwanamke mmoja aliomba talaka dhidi ya mumewe baada ya kasuku kulia kama maharage yaliyomwagika kisha kurudiarudia "Nakupenda" na "Kuwa na Subira".

Mwanamke huyo alirudi toka safari ya muda mrefu alipomsikia kasuku akitoa maneno hayo mara kwa mara mlio wa maharage yanayomwagika kuwa ni mlio wa simu na maneno ya nakupenda na kuwa na subira ni maneno mwanaue huyo alikua akimwambia mchepuko wake.

Mwanamke huyo alimchukua Kasuku huyo hadi kwa wanasheria kwa ajili ya ushahidi mahakamani, lakini wanasheria walisema ushahidi wa ndege haupo kwenye mahakama za China

4.Mwanamke amtwanga talaka mumewe kwa usafi wa kupitiliza
April 2009 Mwanamke wa kijerumani alimpa mumewe talaka kwa kuchoshwa na mumewe huyo kufanya usafi na kusafisha kila kitu wakati wote. Wakiwa na ndoa ya miaka 15, Mwanamama huyo alikia hatua hiyo baada ya kukerwa na mumewe kufanya kazi za ndani na panga pangua ya samani kila mara na hata kuvunja ukuta wa nyumba unaonekana mchafu

5.Mwanaume amtimua mkewe baada ya kudanganywa umria
Huko Shanglin mwanaume mmoja alimtimua mkewe baada ya kuishi nae kwa miaka 10 kwenye ndoa baada ya kubaini alidanganywa umri. Inadaiwa kwamba kabla ya kufunga ndoa mwanamke huyo alimwambia mtarajiwa wake ana miaka 24 lakini baada ya miaka 10 jamaa alipata uthibitisho kuwa awali mkewe alikua na miaka 30 na sio 24 na Mahakama ilikubali uamuzi huo.

6.Mwanamke aomba talaka kwa kutotaka kupata lunch na mama-mkwe kila siku
Huko Romania mwaka 2005 Mrs Elena T. kutoka Foscani kwenye county ya Vrancea aliieleza mahakama ya kwamba uwepo wa mama mkwe kwenye chakula muhimu kila siku imegeuza maisha yake kuwa ya nightmare ndani ya miezi 10 ya ndoa yake. Hata hivyo Mahakama ilimwambie akafikirie upya

7.Talaka la September 11 baada kulipuliwa kwa WTC
Jamaa aliekua na ofisi kwenye floor ya 103 ya world trade center inaonekana aliondoka nyumbani kama vile anakwenda kazini kumbe alikwenda kutumia siku nzima na mchepuko wake nje ya mji na huku kazima simu na hakuna TV wala redio aliosikiliza.

Baadae kawasha simu kuchekicheki msg mara simu ikaita, kapokea mke wake analia akamwambia nakupigia zaidi ya masaa 2 sasa hupokei tunakuhofia upo salama? jamaa kajibu "I'm okey" Wife kauliza tena "Where are you?"
alivo Lafa kajibu, "Where do you think I am? I'm in my office!"


8.Talaka! Baada ya kuishi mwanaume kwa zaidi ya miaka 20 bila mwanaume kujua
Hii nimesoma kwenye kitabu flani hivi. Jamaa mmoja bachela tajiri hivi alikua na tabia ya kwenda kwenye club flan maarufu huko Lagos kuchukua vichangudoa hadi wakamzoea, Baada ya muda akachota kamoja akaweka ndani kabisa akawa wife na ndoa akafunga, katika maisha yao wakajaaliwa kupata watoto 3. Maisha yakasonga kwa furaha .

Miaka 20 baadae jamaa asubuhi akatoka nje akamuangalia mkewe akaanza kumshangaa, akamuuliza "Umefuata nini kwangu?" Mke kajibu "we si mume wangu wa ndoa miaka ishirini sasa na watoto tunao wa3 sasa".Jamaa alipiga ukunga hadi majirani wakajazana akawaambia huyu mwanamke nimeonana nae miaka zaidi ya 20 iliyopita na alikua malaya, sasa leo namuona hapa nashangaa maneno anayoniambia.

Wazee alipombana zaidi yule mwanamke kuna nini nyuma ya pazia ...Kweli yule mama alikiri kuwa ni kweli baada ya kuona hataolewa tena na umri unaenda alienda kwa mganga akapewa dawa ya kupata mume, akaambiwa amuwekee mwanaume yeyote anaemtaka ''Ila kila mwaka ni lazima a renew" na kweli alifanya hivyo ila baada ya kuona ni muda mrefu sana aliona hili jamaa limeshakuwa sugu! Aisee jamaa alitimua mke na watoto wote.


 
Hyo ya mwisho kidogo ifanane na yalionikuta mwaka 2013,sitakuja kusahau !!
 
2.Mwanamke aomba talaka baada mumewe kujaribu kuchungulia na kutaka kuona uso wa mkewe baada miaka 30 ya ndoa
Mwanamke wa Saudia Arabia aliomba talaka mwaka 2008 baada ya mumewe kutaka kuona uso wa mkewe.(Ngoja niulize kwanza..hivi tunapotongoza, tunatongoza watu tusiowaona usoni?) Wanandoa hao waliishi kwa miaka 30 bila ya mumewe kuuona uso wa mkewe. Mke wake huyo mwenye aliekua na umri wa miaka 50 aliishi maisha ya kufuata utamaduni wa asili wa kijijini kwao kusini mashariki karibu na mji wa Khamis Mushayt wa kuficha uso wake wakati wote. Usiku mmoja mume wake huyo alikuja na kujaribu kuinu kitambaa (veil) wakati mkewe kalala ili kuuona uso wa mkewe ghafla mke kashtuka na aliomba talaka papo hapo na ilikua ni kosa lisilopewa nafasi ya kusamehewa japokuwa mwanaume kaomba sana msamaha lakini talaka ilitoka.
imfikie FaizaFoxy wa Mt. Udowe, Br. Lumumba, DSM
 
Namba mbili huyo Dada amekosea Sana halo ameshakua mumewe ana paswa na anahaki ya kumuonesha mmewe sura na mengineyo maaana ameshakua mmewe


Namba NNE sio kweli mwanamke hatoi talaka wala hapaswi kuomba talaka Ila itategemea na mwanaume anakuaje ndan ya nyumba na kutofata sheria wala kumtwii mkewe hapa anaweza kwenda sehem husika(mke) na talaka ikatoka

Mengine hapo juu wala hayana maaana kabisa ni upotoshaji tu.
 
Back
Top Bottom