TAKUKURU yakamilisha upelelezi kesi ya rushwa ya Mbunge Kangi Lugola na wenzake

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imekamilisha upelelezi wa kesi ya rushwa inayowakabili wabunge watatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wabunge hao wa CCM ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ni Ahmed Saddiq (Mvomero), Kangi Lugola (Mwibara) na Victor Mwambalaswa (Lupa).

Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Godliver Kiriani aliiambia mahakama ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na aliomba ipangwe tarehe kwa ajili ya kuanza kuwasomea washtakiwa maelezo ya kesi inayowakabili.

Hakimu Simba alipanga kesi hiyo ianze kusikilizwa Julai 4 baada ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Washtakiwa hao ambao hadi jana hawakuwa na mawakili, wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya Sh5 milioni.

Wabunge hao walipandishwa kizimbani na Takukuru kwa mara ya kwanza Machi 31, 2016 na kusomewa mashtaka na wakili wa Takukuru, Maghela Ndimbo.

Washtakiwa hao wanadaiwa kwa nafasi zao za ujumbe wa LAAC, waliomba rushwa ya Sh30 milioni kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro, Mbwana Magote ili waweze kutoa mapendekezo mazuri ya Taarifa ya Hesabu za halmashauri hiyo za mwaka 2015/2016.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo, Machi 15, 2016, kinyume cha kifungu cha 15 (2) cha Sheria ya Takukuru, wakiwa katika Hotel ya Golden Tulip, iliyoko eneo la Masaki, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
1.JPG
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imekamilisha upelelezi wa kesi ya rushwa inayowakabili wabunge watatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo, Machi 15, 2016, kinyume cha kifungu cha 15 (2) cha Sheria ya Takukuru, wakiwa katika Hotel ya Golden Tulip, iliyoko eneo la Masaki, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam.View attachment 356382
afadhari wakamfunge tupunguze kelele bungeni
 
Hii TAKUKURU ya sasa ilivyomg'ang'ania Mzee Kitilya, nina wasiwasi kama hawa jamaa nao watatoka 'salama'!
 
Hawana hatia hao ni waheshimiwa ndugu yangu.Mwenye hatia yule mwizi wa kuku pale mtaani kwangu na kwako
Mpwa wangu Tetty mwenyezi Mungu ni mwingi wa rehema ipo siku sauti ya mnyonge itasikika.
 
Lugola alilalamika wasikate kiinua mgongo coz ni vihela vidogo alaf wanakata tena,
 
Mpwa wangu Tetty mwenyezi Mungu ni mwingi wa rehema ipo siku sauti ya mnyonge itasikika.

Kuna wakati huwa na Muuliza Mungu,mbona Wanyonge amewaacha sijapata jibu hadi leo.Ukiangalia WalaRushwa,Mafisadi,wezi,Majangili nk nk ndiyo wanaopewa ufalme na ndiyo wanaotumia pesa zao kuhonga ili waendele kuwa wafalme na System inawasaidia ili waendelee kuwa wafalme,Mungu wa Wanyonge kaenda wapi tumfuate??

Kama NEC ingekuwa inauhuru,ingetumia TAKUKURU kuwaondoa wabunge wote wanaopata Ubunge kwa kutumia pesa zao.Lakini leo kesi ya Nyani ati umpelekee Ngedere aamue thubutu.Ione issue ya Kafulila na Wenje,na yule wa Songwe mpaka hakimu anaona aibu kumwambia mtuhumiwa alipwe gharama za kesi.Hatuna mahakimu,mahakimu wengi zaidi ya asilimi 90 ni wale wa pesa kwanza haki baadaye.

Hiyo haki tunaipata wapi??
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imekamilisha upelelezi wa kesi ya rushwa inayowakabili wabunge watatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wabunge hao wa CCM ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), ni Ahmed Saddiq (Mvomero), Kangi Lugola (Mwibara) na Victor Mwambalaswa (Lupa).

Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Godliver Kiriani aliiambia mahakama ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na aliomba ipangwe tarehe kwa ajili ya kuanza kuwasomea washtakiwa maelezo ya kesi inayowakabili.

Hakimu Simba alipanga kesi hiyo ianze kusikilizwa Julai 4 baada ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Washtakiwa hao ambao hadi jana hawakuwa na mawakili, wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza sharti la kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya Sh5 milioni.

Wabunge hao walipandishwa kizimbani na Takukuru kwa mara ya kwanza Machi 31, 2016 na kusomewa mashtaka na wakili wa Takukuru, Maghela Ndimbo.

Washtakiwa hao wanadaiwa kwa nafasi zao za ujumbe wa LAAC, waliomba rushwa ya Sh30 milioni kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro, Mbwana Magote ili waweze kutoa mapendekezo mazuri ya Taarifa ya Hesabu za halmashauri hiyo za mwaka 2015/2016.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo, Machi 15, 2016, kinyume cha kifungu cha 15 (2) cha Sheria ya Takukuru, wakiwa katika Hotel ya Golden Tulip, iliyoko eneo la Masaki, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam.View attachment 356382
tuone kama 'hapa kazi tu' ina ubavu wa kuwatia hatiana wezi wenyewe wa nchi hii. sasa wanalalamika kukatwa kodi gratuity yao huku hawaishi kufanya show bungeni kuidai serikali kuongeza matumizi kila kitu. bora live coverage imefutwa maana ilikua inapalilia unafiki mtupu.
 
Back
Top Bottom