TAKUKURU mnasubiri nini kumkamata na kumchunguza Makonda?

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Nimeona taarifa ya Takukuru ikikanusha kwamba haijamkamata Paul Makonda.

swali wanasubiri nini kumkamata?

@takukuru.tz mimi naomba kusema jambo katika hili.

Sina chuki na Makonda @baba_keagan ila kama mwananchi nina mashaka tuu na utawala wake alipokuwa mtumishi wa umma ,kwamba fedha zetu za umma zilipigwa na kuna dalili zote kwamba fedha zetu za umma zilipigwa akiwa mkuu wa mkoa.

Sabaya alikamatwa sababu kulikuwa na allegations (Tuhuma /Malalamiko) mengi kutoka kwa watu dhidi yake ndio maana akasimamishwa,akachunguzwa na DPP kujiridhisha kwamba ana shutuma za kujibu hivyo kushtakiwa.

Mimi niulize kuna uzito upi kumkamata Makonda ili kuchunguza shutma(allegations) za ubadhilifu na mengine dhidi yake ?

@takukuru.tz Mnataka kusema hakuna viashiria vyovyote vinavyo wapa nguvu nyinyi ya kumchunguza Makonda ?

Sheria ya Takukuru Namba 11 ya mwaka 2007 ,kifungu cha 27 kinasema " Ni kosa mtumishi wa umma kuwa na mali ambazo mwenye nazo hana maelezo ya kuridhisha kuhusu alivyozipata au kuwa na mali au pesa nyingi kuliko kipato chake halali " .

Kwangu mimi binafsi nina wasiwasi na fedha na mali za Makonda, alikuwa na nafasi ya Mkuu wa mkoa tuu.Ila hakuna aliyewahi jua wapi kwingine alikuwa anapata fedha kwa namna alivyokuwa anagawa na kutumia.

Tuhuma za matumizi mabaya ya mamlaka dhidi ya Makonda zilikuwa zinatolewa na watu wengi sana ,Je, takukuru kwanini hamtaki kujiridhisha kama ni kweli au sio kweli juu ya hizo tuhuma?

Mbunge wa Geita vijijini Joseph Kusheku (Msukuma ) tar 7/Feb 2019 alitoa tuhuma Bungeni na kuandikwa kwenye Hansard dhidi ya Makonda,kwamba Makonda ana miliki mali nyingi tofauti na kipato chake akataja Gari Lexus ya Mil.400,magorofa Mwanza, ana miliki magari Toyota V 8 ,alikarabati ofisi yake kwa milion 400 bila kufuata utaratibu wa manunuzi (Chanzo Gazeti la mwananchi tar 8 Feb 2017,J.tano.).

Malalamiko mengine yalitolewa na aliyekuwa Mbunge wa Rombo ,Mh.Joseph Selasini Bungeni tar 11 , Februari 2017 na kuandikwa kwenye Hansard kwamba Makonda ana miliki jengo (Apartment) Viva Towers lenye thamani ya milion 600 ,alimzawadia Gari mke wake lenye thamani ya milion 550 kama zawadi ya Birthday (Chanzo Gazeti la Mwananchi February 11,2017).

Tuhuma zingine zilitolewa katika Blog ya Mtandao ya Sauti Kubwa inayomilikiwa na Ansbert Ngurumo ,mnamo tar 30 Agosti 2018 aliandika na kuambatanisha na nyaraka mbalimbali za umiliki wa viwanja kwamba Makonda ana miliki Ardhi Dodoma eneo la Iyumbu new Town Center viwanja sita jumla mita za mraba 92,341 .

Pia Kugawa gawa fedha.

Tarehe 3/Juni/2019 alitoa fedha kwa wachezaji wa Simba milion 10 kwa Golikipa Manula,milion moja moja kwa kila mchezaji,milion mbili kwa mchezaji wa kike,milion 3 kwa msemaji wa simba @hajismanara na septemba 9,2019 akatoa milion 10 kwa Juma Kaseja ,tar 5 Oktoba 2019 uwanja wa uhuru Dar alitoa Shiling Mil.100 kwa wajumbe wa shina wa CCM Mkoa wa Dar.(Chanzo Millard Ayo na EATV).

@takukuru.tz
mmewahi waza fedha hizi alitoa wapi ? kwamba ulikuwa mshahara wake wa mfukoni ?

Tarehe 18/Septemba/2019 siku ya Jumaano kupitia Gazeti la Mwananchi iliandika kichwa cha habari "Makonda aeleza anakotoa fedha". Makonda kwa kauli yake ya mdomoni baada ya watu kuhoji wapi anapata fedha hizo zote za kugawa gawa ikiwa yeye ni mkuu wa mkoa tuu.

Katika taarifa hii alisema yeye anatumia watu wenye kipato kikubwa kuwaelezea shida na wao hutoa msaada akitolea mfano milion 10 alizompa Juma Kaseja , Makonda alijibu pia nchi hii ni tajiri na watu wake ni matajiri .Kama fedha alikuwa anapewa na wahisani au marafiki je sheria ya inasemaje mtumishi wa umma anapopokea zawadi ? .

Sheria ya maadili ya viongozi wa umma Na. 13 ya 1995 kama ilivyofanyiwa marekebisho kuanzia kifungu cha 12(2 na 3) inaeleza utaratibu wa mtumishi wa umma kupokea zawadi ya zaidi ya thamani ya laki mbili, alipaswa kutoa taarifa kwa muajiri wake lakini pia taarifa ya matamko ya zawadi alizopewa yanapaswa kuwepo katika ofisi ya Kamishna Sekretariati ya Maadili.

Na ndio maana tar 17, Oktoba ,2019 niliandika Barua Sekretariati ya Maadili chini ya Kamishna wa maadili ya viongozi wa umma Marehemu Jaji Mstaafu Harold R. Nsekela nikiomba kukagua Daftari la Maslahi , Rasilimali na madeni pamoja na matamko ya zawadi ya Makonda kama ambavyo kanuni za maadili ya viongozi wa umma za 1996 Na. 168 kifungu cha 6 na 7 kinavyoniruhusu mimi kama Raia kuomba kukagua Daftari hilo.

Barua yangu ilijibiwa tar 15 ,Novemba 2019 ,wakikataa kunipa ushirikiano kukagua Daftari la Makonda nilijua tuu ni kwasababu ya hofu iliyokuwepo na namna Makonda alivyokuwa anaogopwa . Ila suala la kukagua Daftari la mtumishi wa umma katika ofisi ya Sekretariati ya maadili haipaswi kuwa suala la kuomba au la siri, kiongozi akishakuwa mtumishi wa umma tuu kila kitu kuhusu utumishi wake kinapaswa kiwe wazi na umma ujue.

Nitumie fursa hii mara nyingine kwa mujibu wa Sheria ya Takukuru Na.11 ya 2007 kifungu cha 39 kinachonipa mimi mamlaka kama mwananchi kutoa taarifa kwa TAKUKURU popote ninapoona kuna maksio ya uwepo wa Rushwa , kutokana na tuhuma kuwa nyingi dhidi ya Paul Makonda ni vyema TAKUKURU imchunguze na Makonda ili kujiridhisha .

Na kazi ya kuchunguza na kujiridhisha (Prove or disprove the allegations) ni kazi yenu TAKUKURU kama ilivyoelezwa katika sheria ya TAKUKURU kifungu cha 7(e),(f),i,ii,iii, na cha 10 (1) a,b,c .

Sasa tunashangaa kuona mnakanusha kutomkamata Paul Makonda wala kumchunguza.

Abdul Nondo.​


IMG-20210608-WA0493.jpg
IMG_20210608_094852.jpg
 
Jinai inashtakiwa na Jamhuri hivyo hapo ni Jamhuri kuamua kubeba mashtaka na kudeal nayo mahakamani.

Inahitajika presha kulazimisha Jamhuri ichukue hatua na hata ikichukua inaweza muachia vile vile.
 
Je huyu bwanako ZZK ashachunguzwa kwanza au unadhani hatujui mali anazomiliki tofauti na kipato chake?
 
Back
Top Bottom