TAKUKURU mko wapi? UVCCM inateketezwa kwa Rushwa

Pagan Amum

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Posts
1,930
Reaction score
4,409
TAKUKURU mko wapi?, kuna viongozi wa UVCCM na baadhi ya wagombea wataiteketeza jumuiya hiyo kwa rushwa. Tafadhali chukueni hatua za haraka. Rushwa inatembea kama njugu, uongozi umegeuzwa kuwa bidhaa inayonunuliwa sokoni..

Syndicate ya viongozi wakiongozwa na Sadifa, Jokate, Zenda wamegeuza uchaguzi huu kuwa fursa na biashara ya kujipatia kipato. Wagombea wao nao wanazunguka mikoani na kutoa rushwa ya kufuru... Baadhi yao ni
1. Jackson Kangoye
2. Kheri James
3. Abdul Van Mohamed
4. Suleiman Serera
5. Ayoub Tesha
6. Sophia Kizigo
7. Mathias Kipara

Kwa sasa wanaendelea kutembea mikoani na wilayani na kutoa rushwa ya kufuru. Tunashukuru juzi moja kati yao alikamatwa na ofisi zenu za Katavi akiwa anagawa rushwa..

NB:. Hii vita ya rushwa ni kubwa. Ni jukumu letu kumsaidia Rais wetu mpendwa Magufuli
 
Kama una taarifa kwa nini usiwapelekee Takukuru? Isije kuwa nia yako kuwachafua wahusika.
 
Ndugu wakigombana chukua jembe kalime, wakipatana wewe unavuna; au tuseme Mambo ya Ngoswe.......
 
Unadhani wanatoa wapi hzo pesa mkuu? Wale walioripotiwa kaskazini wamefanywa nn?
Tumuombe Mungu tu!
 
Unadhani wanatoa wapi hzo pesa mkuu? Wale walioripotiwa kaskazini wamefanywa nn?
Tumuombe Mungu tu!
 
UVCCM iliondoka na Nchimbi!!
 
takokuru wao wanakaa tu,ofisini wanasubiri waletewe wala rushwa,wakiambiwa mahala Fulani kuna rushwa hawaendi kwa mfano pale stend ya Arusha rushwa inatolewa waziwazi lakini awaendi eti wanasubiri wapelekewe ushaidi wakiwa maofisini, hawataki kabisa kuwa mashaidi kwa kuona wenyewe
 

Mbona kuna mmoja hapo umemsahau Mkuu? au labda ndiyo Wewe mwenyewe hivyo baada ya kuona umezidiwa na hao Watajwa wako hapo ndipo ukaamua uje uwaanike huku? Huyo uliyemuacha hapo katika hiyo list yako ndiyo anahonga kupita maelezo halafu anakumbatiwa kuanzia na Mamlaka ya Mkoa wa Dar es Salaam hadi Mamlaka nzima ya Magogoni Feri. Nakupa tu initials kisha utajiongeza mwenyewe ambazo ni JRM. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…