TAKUKURU: Lazima tutashinda vita ya rushwa

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imemuahidi Rais John Magufuli kufuata nyayo zake kwa kutangaza vita dhidi ya rushwa huku ikisisitiza kwamba lazima watashinda.

Kwa upande wake Rais Magufuli, amepongeza mwenendo wa utendaji wa taasisi hiyo na kusema kwa kasi ambayo TAKUKURU inakwenda nayo, inamtia moyo na kuna kila dalili kwamba Tanzania itafika mahali pazuri.

Akizungumza mara baada ya kumkabidhi ripoti ya utendaji ya taasisi hiyo kwa mwaka 2014/15, Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Valentino Mlowola, alisema kupitia hotuba ya Dk Magufuli aliyoiwasilisha wakati akifungua Bunge Novemba mwaka jana, taasisi hiyo imepokea kwa vitendo tangazo la kupiga vita rushwa.

“Kama TAKUKURU, tuna jukumu la kuratibu mapambano dhidi ya rushwa ili Watanzania wapate haki na maendeleo. Tunatambua rushwa ni adui wa haki na maendeleo kwa nchi yoyote ile. Ndiyo maana TAKUKURU tumeipokea hotuba ile kama tangazo la vita dhidi ya rushwa,” alisema Mlowola.

Alisema taasisi hiyo itaendelea kuwajibika kwa kusambaza elimu kwa wananchi dhidi ya tatizo la rushwa lakini pia itachukua hatua za kisheria dhidi ya wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

“Nakuhakikishia mheshimiwa Rais wananchi wanatuunga mkono dhidi ya vita hii na nakuahidi kwa dhati kabisa tutashinda vita hii,” alisisitiza. Akizungumzia ripoti hiyo, alisema imejumuisha utendaji mzima wa taasisi hiyo kwa mwaka huo, changamoto, mafanikio na matarajio yanayoongozwa na hotuba ya Rais ya uzinduzi wa Bunge.

Alisema ripoti hiyo ilitarajiwa kuwasilishwa kwa Rais Magufuli tangu Machi mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya TAKUKURU, lakini kutokana na Rais huyo kuwa mapumzikoni, ndio maana imewasilishwa kwake jana.

Akizungumzia taasisi hiyo, Dk Magufuli alisema ameipokea ripoti hiyo na kuahidi kuisoma na kuziangalia changamoto zilizoainishwa kwa ajili ya kuangalia namna ya kuzipatia ufumbuzi.
 
ZINATAFUTWA SIFA ZA KIJINGA TU HAPO! WAKATI CCM WANAHONGA WAPIGA KURA MLIKUWA WAPI?! WALE MASHAVU TU!
Mbona umewasahau waliokuwa wakihongwa mafuta ya bodaboda na viroba? Rushwa ni adui wa haki iwe CCM au UKAWA, haifai tuungane na Magufuli kupambana nayo
 
Ni wakati sasa takukuru wanatakiwa ku walk the talk. Tumechoka na porojo, ni jana tu nimelazimishwa na traffic kutoa rushwa ya shs 5,000- na jamaa hana hata aibu kaisunda mfukoni shaaaaaa
 
Back
Top Bottom