Jana kwenye taarifa ya habari nilimuona Dr. Hosea wa TAKUKURU akifungua jengo huko Karatu (sikumbuki vizuri) la thamani ya millioni 900 na kuahidi kujenga mengine matatu sijui wapi. Picha ya haraka niliyoipata ni kuwa kumbe rushwa haitakaa iishe, inabidi ijengewe maofisi mengi tu nchini. Hii ina maanisha kuwa mafisadi wataendelea kuwepo muda wote bila mabadiliko? Ningekuwa kiongozi ningerudisha AZIMIO LA ARUSHA hata kesho, tena lifundishwe mashuleni kuanzia chekechea. Yani nchi imekosa maadili namna hii jamani?