Takukuru iringa mna nini na mwakalebela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takukuru iringa mna nini na mwakalebela

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lutala, Mar 10, 2011.

 1. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35

  Aliyekuwa mshindi katika kura za maoni ndani ya CCM katika jimbo la Iringa mjini kupitia CCM Frederick Mwakalebela na mkewe Celina leo wameachiwa huru na mahakama ya hakimu makzi Iringa katika kesi yao ya rushwa katika mchakato wa kura za maoni baada ya mahakama hiyo kubaini kuwa hawana kesi ya kujibu.

  Leo mahakama hiyo ilikuwa ikitoa maamuzi madogo ya kuendelea ama kutoendelea katika kesi hiyo ambayo ilifunguliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru ) mkoa wa Iringa.

  Hii ni mara ya pili sasa Mwakalebela kuishinda Takukuru mahakamani hapo. Hivi karibuni Mahakama hiyo ilimwachia huru Mwakalebela kabla ya Takukuru kumfungulia tena kesi.

  Hata hivyo wengi wamekuwa wakihoji sababu ya Takukuru Iringa kuendelea kung'ang'ania kesi hiyo huku watuhumiwa wengine wakiachiwa na mahakama bila kusumbuliwa kama ambavyo Mwakalebela anasumbuliwa na taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana na rushwa kubwa na ndogo ndogo. (source: Francis Godwin)
   
 2. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hivi hawa watuhumiwa kushinda kesi tatizo ni mfumo wa sheria au serikali ina wanasheria wachovu ambao hawana uwezo wa kushinda kesi?
   
Loading...