mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,410
- 4,988
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Bukombe, mkoani Geita, imetoa rai kwa mawakala wa miamala ya kifedha kuchukua tahadhari na kufuata sheria na miongozo ya kazi zao, hasa kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, ili kujiepusha kutumiwa na wagombea, wapambe wa wagombea kuwatumia mawakala kutoa rushwa kwa wapiga kura.