Takribani Wanafunzi 2,700 Vyuoni waingia mitini kuhakikiwa Bodi ya Mikopo

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
Wanafunzi 2,739 mbalimbali hawakujitokeza kuhakikiwa wakati Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ilipofanya shughuli hiyo katika vyuo 26 nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa bodi hiyo, Jerry Sabi amesema taarifa hiyo ni ya awali baada ya uchambuzi taarifa za uhakiki wa vyuo 18 kati ya 26 vilivyohakikiwa.

Amesema bodi hiyo imetoa siku saba kuanzia leo kwa wanafunzi ambao hawajahakikiwa kujitokeza ili wahakikiwe vinginevyo wataonekana kuwa ni wanafunzi hewa.

Amesema Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ndicho kinachoongoza kuwa na wanafunzi wengi wasiohakikiwa wanaofikia 763.
 
Kwani hiyo bodi haina takwimu kamili za wanafunzi wanaopewa mikopo,mpaka wapitishe lokoo ya mtu mmoja mmoja? Tz lini dijitali itawini kimatumizi?
 
au hawana sifa ya kupata mikopo kwaio wanaogopa kuumbuka ?, uongozi wa chuo ndyo unatakiwa kubanwa kutoa taariza zaid apo
 
Wanafunzi 2,739 mbalimbali hawakujitokeza kuhakikiwa wakati Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ilipofanya shughuli hiyo katika vyuo 26 nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa bodi hiyo, Jerry Sabi amesema taarifa hiyo ni ya awali baada ya uchambuzi taarifa za uhakiki wa vyuo 18 kati ya 26 vilivyohakikiwa.

Amesema bodi hiyo imetoa siku saba kuanzia leo kwa wanafunzi ambao hawajahakikiwa kujitokeza ili wahakikiwe vinginevyo wataonekana kuwa ni wanafunzi hewa.

Amesema Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ndicho kinachoongoza kuwa na wanafunzi wengi wasiohakikiwa wanaofikia 763.
Na hawa madogo wa special diploma waliofukizwa wao watahakikiwa wap na nan?
 
Hapa ndio kwenye mtego, baada ya kujua wanafunzi hewa ni wangapi litakuja swala la wamezalishwaje? Na hela inakwenda wapi? Wataingia waliokuwemo na wasiokuwemo. Vyuo vina madeski ya mikopo-sasa haya yanatokeaje?
 
Mkuu hiyo mm naipinga kwa asilimia zote, ili mtu apewe mkopo bodi inajiridhisha naye ndio apewe huo mpunga sasa leo anakosaje vigezo?
Kwani hukusikia viongozi wa HESLB kufukuzwa/kusimamishwa kazi kutokana na uzembe /makusudi kuwapa mikopo wanafunzi wasiostahili na kuwanyima wanaostahili
 
Back
Top Bottom