Ni ngumu sana kwa bongo, kwa sababu mambo mengine yanaanzia kwenye utaifa na elimu ya uraia. Waweza kuniambia kwamba naingiza siasa lakini wakati mwingine pamoja na kuwa ustaraabu ni hulka ya mtu. Jamii ya watu miongoni mwao wamekata tamaa huwa hawana cha kupoteza. Mfano mzuri utauona kwenye uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa vyanzo vya maji, wapo watu wanaofanya hivi kwa makusudi na ukitokea kumuona na kumuuliza atakwambia atunze chanzo cha maji wakati hata hiyo kesho hajui kama ataiona (kwa kukosa chakula cha leo). Hivyo hivyo katika kujidaidia hovyo mifano ni hiyohiyo.
Ni mawazo tu, miongoni mwao watanzania tupo.