Kuna mdau keshakujibu hapa.
Tairi confortable zaidi
Kama unataka tairi pana kwa ajili ya show nzuri na stability barabarani recomended size ni 225/60/R16
Au 225/55/R16 ila hii inashusha gari kidogo kama unatumia rough road itakupa shida kidogo.
Pia size 235/50/R17 ni tairi pana kidogo recomended na Subaru wenyewe.
Zingatia ukitumia tairi ya size 225 au 235 lazima rim yako iwe size 7.5J.
Kwa kuwa Forester ni gari yenye nguvu (torque) unatakiwa kununua brand nzuri kwa dealer kama vile Kumho, Good year, Michelin, Pirreli. Etc.
Achana na mchina wa bei nafuu utakula hasara ndani ya miezi 6.