TAIFA STARS HII KWA BUKINAFASO YA AFRICON BORA YA TANZANIA PRISON.

katichi

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
2,011
1,179
Michezo ya ufunguzi ya kombe la mataifa ya Africa imeanza rasmi jana uko nchini Gabon kwa michezo miwili.
Michezo wa Kwanza ulikuwa baina ya wenyeji Gabon iliyo chini ya naodha Aubemeyang ambaye pia anaichezea B. Dortmund ya nchini Ujerumani na timu ya Taifa ya Guinea Bissau ambapo walitoka 1- 1.

Mechi ya pili iliyoanza mida ya usiku kwa saa za Africa ya mashariki ilishuhudiwa pambano zuri la vijana walio kamilika kila Idara kuanzia maumbile yao marefu,nguvu pamoja na ufundi kwa kiwango fulani.

Kilichonivutia katika pambano hili la pili ni jinsi wachezaji wa timu zote mbili za Cameroon na Bukinafaso walivyo na utimamu wa miili pamoja na akili .Nikavuta picha kwa TAIFA STARS yetu hii tuliyonayo kweli inaweza kufua dafu kwa Bukinafaso licha ya kwamba tuliwahi wafunga kwao kipindi fulani nimetafakali nimekosa majibu labda maana mpira wetu huu ninavoujua wa kucheza mchezo mlaini sijui ingekuwaje.

Pekee naona ni bora tungeichukua timu ya Tanzania Prison wanajela hela hawa kutoka green city wangejaribu kidogo kwa mchezo wa Jana maana wengi wa wachezaji wa timu hii wanamiili pande nne na warefu wa kutosha na wanacheza kwa kutumia nguvu.

Karibuni kwa tathimini yenu.
 
mkuu wale Serengeti wako vizuri na hata cjui wameishia wapi, wanaweza kupambana walee
 
Kiukweli hata mimi nilishangaa kuona wachezaji warefu na wenye miili yakutosha.Nikawaza kama wewe.Kwamba ikipigwa kona tutaambulia chochote kweli?
 
haaaaaaa, labda tuwanyweshe Serelaki. Ili wapate Mwili wa kupambana.
 
kwa kiwango cha mpira kilichoonyeshwa na Tim zote kwenye mechi za ufunguzi kimenipendeza sana....tunaitaji muda sana kuwa kama wale wenzetu..."sisi sio wale wala Wa kesho"Cameroon wamecheza vizur sana wamefunga kiufundi sana.
vile vile Burkina Faso wamecheza vizuri...na wamesawazisha goli kiufundi pia....@Natumain AFCON itakuwa na ladha yenye vionjo vitamu..
 
mkuu wale Serengeti wako vizuri na hata cjui wameishia wapi, wanaweza kupambana walee
Mkuu kwa mechi ya Jana bado sana tunahitaji wachezaji angalau karibia asilimia 80 wenye miili pande nne hapo tutafika
 
Kiukweli hata mimi nilishangaa kuona wachezaji warefu na wenye miili yakutosha.Nikawaza kama wewe.Kwamba ikipigwa kona tutaambulia chochote kweli?
Uliona kumbe ndo mana nimesema bora Tanzania Prison wangejaribu
 
kwa kiwango cha mpira kilichoonyeshwa na Tim zote kwenye mechi za ufunguzi kimenipendeza sana....tunaitaji muda sana kuwa kama wale wenzetu..."sisi sio wale wala Wa kesho"Cameroon wamecheza vizur sana wamefunga kiufundi sana.
vile vile Burkina Faso wamecheza vizuri...na wamesawazisha goli kiufundi pia....@Natumain AFCON itakuwa na ladha yenye vionjo vitamu..
Kweli Mkuu
 
Kwani Messi/Walcot wana wana maumbo makubwa?,..Ufundi kwanza ambao wachezaji wetu hawana.
Unaweza ukawa na umbile dogo lakini kama ulipata lishe nzuri toka mdogo unakuwa na mifupa iliyojengeka vizuri, hata uzito huwa tofauti na umbile. Wachezaji wetu wepesi mno.
 
Back
Top Bottom