Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,685
- 149,894
Mimi huwa najiuliza sana sisi watanzania kwa ujumla wetu kama Taifa tumefanya nini kutambua uthubutu wa wabunge hawa vijana wa kutokupokea sitting allowance?
Wengi wetu tumekuwa vinara wa kupinga hii posho lakini sijaona juhudi zozote za kitaifa za kutambua na hata kuwapongeza wabunge hawa waliothubutu kuacha kuchukua posho hizi na badala yake wameamua kuziacha zikafanye kazi nyingine.
Raisi Magufuli kila hatua anayochukua ya kubana matumizi amekuwa akimwagiwa sifa kemkem kuanzia ndani ya chama chake mpaka kwa viongozi wa dini.Cha ajabu, si viongozi wa dini wala chama chake cha CCM kimewahi kumpongeza Kingu kwa uamuzi wake huu.
Halikadhalika,si chama chake cha sasa cha Zitto(ACT) wala chama chake cha awali (CHADEMA), wamewahi kumpongeza Zitto kwa uamuzi wake huu achilia mbali viongozi wa dini na Taasisi zingine zikiwemo za wanaharakati.
Raisi Magufuli,kama mbana matumizi,naye hajawahi hata siku moja kumpongeza Zitto wala mbunge wa chama chake mh.Kingu kwa kubana matumizi.Kukaa kwake kimya kuhusu jambo hili kwakweli huwa simuelewi!
Sasa najiuliza kama tumeshindwa kutambua uthubutu wa wabunge hawa wawili,tunatarajia hawa wabunge wengine wanaoendelea kutafuna posho hizi wafanye nini zaidi ya pengine hata kudai posho hii iongezwe?
Leo hii Magufuli akitangaza kuwa posho fulani kuanzia leo hii nitakuwa sichukui.Je,habari hiyo haitakuwa wimbo wa Taifa?CCM hawataacha kumpongeza?Viongozi wa dini hawataacha kumpongeza?Wanaharakati nao hawataacha kumpobgeza bila kusahau na vyombo vya habari?
Hivi sisi kama Taifa kweli tunajitambua?Nini hasa tunachokisimamia kama watanzania kwa ujumla wetu?Posho hizi za wabunge wawili zinaweza kuonekana kama ni jambo dogo lakini mtazamo huu ndio "reflection" ya uzalendo wetu kama watanzania.
Zitto na Kingu,pamoja na mapungufu yenu, hongereni sana kwa uamuzi wenu huu mgumu na wa kizalendo maana siku zote pesa huwa haitoshi.
Wabunge wengine oneni aibu na muwaunge mkono hawa wabunge wenzenu badala ya kuwakatisha tamaa kwa kuwapotezea kama mnavyofanya.
Ningekuwa Magufuli(Raisi mbana matumizi) shariti mojawapo la mtu kuwa waziri kwenye serikali yangu ni awe tayari ku-sacrifice posho hii na si vinginevyo.